Wanaume Korea Kaskazini wanakabiliwa na mtihani mpya katika taifa lao; wa kunyoa nywele kwa mtindo ulioamuliwa na rais wao.
Watake, wasitake kuanzia sasa kila mwanamume atalazimika kunyoa nywele zake kwa mtindo anaoupenda Rais Kim Jong- un.
Kiongozi huyo kijana, aliyerithi wadhifa huo baada ya kifo cha baba yake, hana mzaha hasa kutokana na nia yake ya kujenga mfumo mpya wa utawala ambao matakwa yake tu ndiyo ya kufuatwa.
Ni wiki mbili sasa tangu serikali ya nchi hiyo kutoa agizo linalowataka wanaume kunyoa kama rais wao, huku wanawake nao wakielekezwa kutengeneza nywele zao kwa aina 18 tofauti na si zaidi ya hapo.
Hilo ni moja ya maagizo yenye utata kuwahi kutolewa chini ya utawala wake, ambapo amekuwa akifanya jitihada za kujijengea mizizi, ikiwamo kuwaondoa na kuwaadhibu wale waliokuwa katika utawala wa baba yake wanaoonekana kutokubaliana na aina yake ya uongozi.
Huu ndio ubaya wa kuwapa madaraka watoto wadogo, wakishavuta bangi wanayowaza ndio hayo hayo
ReplyDeleteKaazi kwelkwel mbona hawapendezi kama banda la nyasi lililozeeka linataka kuanguka.
ReplyDeletehuyo jamaa hanaga mzaha kabxa,alimnyonga mjomba wake hv hv
ReplyDeleteKwani umoja wa mataifa hawalioni hilo?
ReplyDeleteau wamerizika nalo mbona hata picha inamuonesha ni mdogo je xaxa sheria mpaka ihamie kwenye nywele hata m2 mstarabu anyoe kiduku duuhh!!! majananga.
Tabia hz ndo wanazotuletea ccm hapa tz, kulazimisha matakwa yao bila ya wananchi kutopenda , inakera sana, sijuwi ni kukosa ustaarabu au elimu ndogo au ni udikteta ? Ukwel kwmba mnaudhi sana nyie jamaa hata MUNGU hapendi tabia hz za kijinga
ReplyDeletehizi ni bangi za kuvutia chooni mbaya kweli kweli tungoje akili yake irejee
ReplyDeleteeh kweli aise labda tu msubiri akili yake irejee
ReplyDelete