WAPINZANI NA SWALA LA SEREKALI TATU..KUNA NINI?


Kwanini wapinzani wamenga'nga'na sana na swala la serikali tatu? Ni kweli ni kwa ajili ya maslahi ya watanzania au maslahi ya kisiasa?

Wapinzania hawajawahi kuwa pamoja kwenye maswala ya msingi wala hata kuungana tu kwenye chaguzi ili kutengeneza nguvu ya kuing'oa CCM, ila hapa kwenye serikali 3 wamekua pamoja hasa?

Kwenye kampeni za Lipumba misikitini anawaponda CHADEMA, na CHADEMA wanafahamu hilo, yaani hawa jamaa nje ya malumbano ya serikali 3 ni maadui.

Kwanini tusilazimishe serikali 1 au turekebishe makosa yaliyopo?

USA ilinunua Alaska na New Mexico ili kujiongezea rasilimali watu na ardhi, Huyu Nyerere ambaye wapinzani wanajidai kumuenzi alisema ili tuendelee tunahitaji WATU, ARDHI, SIASA SAFI NA UONGOZI BORA.

Hapa tunachokosa ni SIASA SAFI NA UONGOZI BORA sasa tuna sababu gani ya kupunguza ardhi na rasilimali watu?

Tukirekebisha kasoro za muungano na wapinzani wakasimamia maswala ya msingi ya nchi hii ambayo CCM wamekua wakibabaisha kama UFISADI ULIOKITHIRI, RUSHWA ELIMU DUNI NA MENGINE LUKUKI TUNAYAFAHAMU.

Nitakuwa wa mstari wa mbele kwenye maandano yatakayoitishwa na wapinzani. Hili la serikali 3 likifanikiwa we will be the f***in' loosers.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Acha ukada wewe!

    ReplyDelete
  2. Kasoro za muungano hazirekebishiki kila
    Siku tukienda mbeke zinaongezwa na walafi wa madaraka wanaotaka kujikusanyia kila kitu kiwe ktk milki yao. Tokea kero imeanza moja sasa zimefikia mia moja kweli walikua hawaoni au wanafanya kwa kukusudia hao.

    ReplyDelete
  3. Muungano uvunjwe...thats the solution.
    Wakitaka waanze upya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad