MWENYEKITI wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amezima rasmi sakata la makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kulazimisha Bunge Maalumu la Katiba kukataa pendekezo la Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu muundo wa Muungano wa serikali tatu.
Akiwasilisha Rasimu ya Pili ya Katiba bungeni jana, Jaji Warioba alisema uchambuzi uliofanywa na tume yake umezingatia maoni ya wananchi, historia na hali halisi, na kwamba ili muungano udumu serikali tatu hazikwepeki.
Alisema tume ilitafakari maoni mbalimbali yaliyotolewa na wananachi na makundi, na ilirejea ripoti kadhaa za miaka zaidi ya 20 mfululizo, ikazingatia malalamiko ya Zanzibar na Tanganyika, mgongano wa kikatiba kati ya Katiba ya Zanzibar na ya Muungano, na mengine mengi.
fanya kazi yako babu yng achanananao hao inzi wa kijani
ReplyDeleteBabu warioba size ya surual na koti & shoes pleas, niko thailand chuo, mwezi wa saba narudi, lazima nikuletee, hv blessed my grandfather
ReplyDeletemi navaa kia2 namba 39 kiuno 28 hips 42 naomba n mm nletee bas
Deletebaba wafundishe vijana hao, na wape maadili ya enzi zenu ili nchi irudi kwenye mstari, watu wasitajirike kwa wizi!!!
ReplyDeleteKwanin babu usigombee urais? Kula yangu ntakupa
ReplyDelete