ALICHOSEMA JUX BAADA YA UMBEA KUZAGAA KUWA AMEFANYA VIDEO NA JACK CLIFF

December 2013 zilitoka stori kwamba Mtanzania Jackie Cliff ambae ni mrembo aliewahi kutokea kwenye video kadhaa za wasanii wa bongofleva amekamatwa na dawa za kulevya huko China.
Jackie Cliff ni mpenzi wa msanii wa bongofleva aitwae Jux ambae amehojiwa na Gossip Cop Soudy Brown baada ya picha kadhaa kusambaa akitengeneza video yake mpya huko China na mrembo ambae hajaonekana sura, ishu ambayo imefanya wengi wahisi kwamba ni Jackie Cliff.
Jux amekanusha stori kwamba hivyo video amefanya na Jackie Cliff na kusisitiza kwamba kutomuweka Jack kwenye hiyo video ni kutokana na sababu zake binafsi na wala hataki kuzungumza zaidi kuhusu hizo ishu.
Namkariri akisema ‘siwezi kusema ila kama atakuepo kwenye video au hatokuepo… ni watu wenyewe wataona’
Kwenye sentensi nyingine Jux amekanusha stori za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Vanessa Mdee ‘V money’ kwamba ni rafiki yake tu ila hakuna kingine cha zaidi’

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad