BAADA YA KUSUSIA BUNGE WAJUMBE WAIMBA NYIMBO HIZI" UKOMBOZI NI SASA, VIJANA MSILALE BADO MAPAMBANO"

Nje ya Ukumbi wa Bunge, wajumbe hao kutoka Ukawa na baadhi ya wajumbe kutoka kundi la wajumbe 201 walioteuliwa na Rais, walitoka wakiimba “CCM Interahamwe”.

Pia walitumia falsafa maarufu ya Mchungaji Mtikila ya “Saa ya ukombozi ni sasa,” kuchagiza safari yao ya kutoka Ukumbi wa Bunge Maalumu la Katiba hadi Ukumbi wa Pius Msekwa uliopo eneo hilohilo la Bunge.

Wakiwa ndani ya ukumbi huo, wajumbe hao waliendelea kuimba nyimbo mbalimbali ikiwamo wimbo wa mshikamano (Solidarity forever) unaoimbwa na wafanyakazi kuonyesha mshikamano.

Pia waliimba: “Vijana msilale bado mapambano... Ukawa msilale bado mapambano.” Halikadhalika, wajumbe hao waliimba nyimbo mbalimbali za kumshutumu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi na baadhi ya nyimbo hizo zilisikika “Lukuvi mbaguzi” na “Lukuvi mchochezi.”

Interahamwe ni kikundi cha wanamgambo wa Kihutu wa Rwanda ambacho kilichochea mbegu za ukabila na kusababisha mauaji ya halaiki ya Rwanda dhidi ya Watutsi.

Wajumbe hao walitoka nje ya ukumbi huo wa Bunge la Katiba wakiongozwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa vyama vya siasa akiwamo Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF na Freeman Mbowe wa Chadema.

Viongozi wengine wa kitaifa ni Emmanuel Makaidi wa NLD, James Mbatia wa NCCR-Mageuzi na Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na viongozi wa vyama vingine ambao majina yao hayakupatikana.

Ndani ya Ukumbi wa Msekwa, Profesa Lipumba aliwashukuru wajumbe wote waliowaunga mkono wakiwamo baadhi kutoka kundi la 201 na kueleza kuwa kauli ya Lukuvi ndiyo kiini cha mgogoro huo mpya wa kisiasa. Alivitaja vyama vingine vya upinzani vilivyowaunga mkono kuwa ni NRA, Chauma na UDP.

“Imebidi tutoke… kwa namna tulivyokuwa tunakwenda ilikuwa hamna tija yoyote na hatuwezi na sisi kuungana nao (CCM na makundi yaliyobaki) kufanya maasi dhidi ya Watanzania,” alisema.

Profesa alipendekeza wajumbe wote wakutane leo saa 4:00 asubuhi kwenye Ukumbi wa Hoteli ya African Dreams ili kujadili na kuweka msimamo wa mwelekeo wa baadaye wa umoja huo.

Profesa Lipumba alisema baada ya kikao cha leo, watakwenda mapumziko ya Pasaka na hawatahudhuria tena mkutano huo wa Bunge la Katiba hadi mwafaka wa kisiasa utakapopatikana.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Good tupiganieni wa kuu achaneni na hao interahamwe kumanina zao.wajali matumbo yao na ya paka zao tu fucken..

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bila shaka ubongo wako umejaa kamasi. La sivyo utakuwa unatumia mkundu kufikiri

      Delete
    2. Hiyo comment iliyotangulia ya matusi imetoka kwa Mwigulu Nchemba.

      Delete
    3. Sasa kulikuwa na haja gan ya kumtukana na wakati wew mwenyewe unaona kabisa mustakabal wa nchi hii unavyo kwenda ndugu!nahdan wewe ndio ubongo walo umejaa kamas na unafikiria na mkundu shwain kabisa!utakufa na umasikin wako kazi kushabikia mafisad!nchi hii ina wenyew wew mtoto wa fundi bomba.

      Delete
  2. hawa wabunge they luck respect to themselves they speak nonsense r of no importance in this country rest in peace tz parliament

    ReplyDelete
  3. Watanzania mlisha aambiwa namna akili kila kitu mnafanyiwa. mmetoa maoni wanasema ni kipuuzi wao wanataka cah kutoka chama chao na mkikataa mtafute kwa kwenda au nchi itachukuliwa na jeshi, Zanziba huru tanganyika hakuna, mnadai Tanganyika mnaijua? ndio upuuzi tunaambiwa, Wanasema Serikali tatu gharama wakati wana Mawaziri wasio kuwa na Wizara si ujinga huu?

    ReplyDelete
  4. Haya bana ngoja nirudi Dubai after Easter nikachape kazi hku naona nyota tuu bora nikaendelee kukaa kwa waarabu nijitafutie kipato.huku ntawasoma tu na maigizoyao basi

    ReplyDelete
  5. Ccm ni maharamia wasio na huruma kwa wananchi wa tz

    ReplyDelete
  6. Jaman ss huo muafaka mtaupata vp bila majadiliano mmetoka bungen muafaka utatoka wap nyie wasenge manyoya rudin mbungen kumnina zenu nyie pa mapumbu yenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. We bahati inaonesha akili yako ndogo Sana au Ni mvivu WA kufikili

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad