BONDIA Francis Cheka ametajwa kuwa mwanafunzi anayeongoza kwa kukacha vipindi vya darasani chuoni anakosoma huku mwalimu wake, James Mkisi akibainisha kuwa kutokana na utoro wa bondia huyo hata kiti na meza yake darasani vimeanza kuweka kutu.
Cheka alipewa ofa ya masomo na Chuo cha St Joseph cha mjini Morogoro mwezi mmoja baada ya kutwaa taji la Dunia la WBF Agosti mwaka jana kwa kumpiga Phil Williams wa Marekani jijini Dar es Salaam.
“Inavyoonekana Cheka hataki shule, tangu tumempa nafasi hii aliingia darasani siku moja na hakuonekana tena, mwezi uliopita alikuja akatuambia sasa anahitaji kusoma, tukamsha§uri aanze upya muhula ulioanza Machi kwa kuwa wenzake walimuacha.
“Baada ya hapo hakuonekana tena, huyu mwanafunzi anatuchanganya sana inaonekana hataki kusoma ukizingatia alishakuwa bingwa wa Dunia,” alisema mwalimu Mkisi.
Alisema hata uwaziri wa michezo aliokuwa amepewa hivi sasa cheo hicho kinakaimiwa na naibu wake baada ya Cheka kutoonekana kwa miezi kadhaa sasa na kubainisha kuwa bado nafasi waliyompa ipo palepale hadi mwishoni mwa mwaka huu kama hajatokea shauri yake.
Cheka alikiri kutokwenda shule na kusema kuwa alibanwa na shughuli za kifamilia kama baba ingawa anajipanga kuanza masomo yake ya kompyuta, biashara na lugha aliyopangiwa kusoma chuoni hapo.
atawabonda huko darasani mpaka mshangae
ReplyDeleteHapana Msomaji hapo
ReplyDelete