BONGO MUVI KWAWAKA MOTO

Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan

PENYE wengi pana mengi! Lile kundi la mastaa waigizaji wa Kibongo, Bongo Movie Unity, linadaiwa kuparanganyika baada ya kuwaka moto kufuatia mwenyekiti wao, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’ kudaiwa kuwa na upendeleo kwa baadhi ya wanachama wa jinsia ya kike.

Habari za uhakika kutoka kwa chanzo makini ndani ya kundi hilo zilieleza kuwa mwenyekiti wao huyo amekuwa na tabia ya kuwaburuza wanachama wake kama magari mabovu huku wakishindwa kubishana naye kwa lolote hivyo kila kitu anapanga mwenyewe kwa akili zake na anataka kiende kama anavyotaka.

Chanzo hicho kilidai kwamba mfano halisi ni hivi karibuni ambapo wasanii hao walikuwa wakisherehekea miaka mitatu tangu kuanzishwa kwake, Steve alipanga kila kitu mwenyewe pamoja na kwamba walichagua kamati lakini hazikufanya kazi yoyote.

“Jamaa anaamua vitu mwenyewe, halafu anatupeleka sisi wanachama kama gari bovu, sasa angalia ndani ya kundi hakuna maelewano, wanachama wengine wameamua kujitoa kama Ray (Vincent Kigosi), ameshajitoa pia mmoja wa waanzilishi Jimmy Mafufu amejitoa, sijui ataishia wapi huyu mwenyekiti na uamuzi wake,” kilisema chanzo hicho.

Wanachama mbalimbali wamekuwa wakilalamikia kitendo cha mwenyekiti wao kutoa tuzo kwa wanawake anaodaiwa kuwa nao, badala ya kutoa kwa wale wanaofanya vizuri kweli.

“Eti kama yule msanii aliyempa tuzo ya kwamba anajiheshimu anayeitwa Mille ana heshima gani, ameacha kumpa mwanzilishi wa kundi hilo hata kumpongeza tu na kwenda kuwapa hao huku wakimweka nyuma kabisa mwanzilishi ambaye ni Jimmy Mafufu jamani tunaenda wapi,” kilisema chanzo.

Akizungumza kwa masikitiko juu ya sakata hilo, Mafufu alisema anaumizwa na tabia ya viongozi kuonesha roho mbaya na ubinafsi kwani siku ya ‘bethidei’ ya Bongo Movie Unity hata hawakumkumbuka kwenye tuzo yoyote hata pongezi ya mdomo haikuwepo.

“Mimi ndiye niliyeanzisha Bongo Movies Unity, hakuna kundi ambalo limeshawahi kudumu kama hili hivyo haikuwa kazi rahisi kwangu lakini viongozi hawalioni hili wanaingiza roho mbaya na ubinafsi.
“Roho inaniuma sana mimi ndiye niliyewapa fomu wanachama wote na vitambulisho vyote vina saini yangu lakini leo naonekana sijafanya la maana, niko kwenye hatua za kujitoa kwa sababu sioni faida ya kukaa na watu wasionisapoti.

Ili kupata mzani wa habari hiyo, gazeti hili lilimmwagia ‘upupu’ wote Steve Nyerere ambapo alikuwa na haya ya kusema: “Tuhuma hizo siyo za kweli, tuzo nilitoa kwa wasanii wachanga ili kuwapa moyo wa kufanya vizuri zaidi.

“Kuhusu Jimmy Mafufu, nautambua sana mchango wake sema tu ana haraka na hao wanaosema nawapeleka kama gari bovu, wanakosea kwani najitoa sana, natumia muda mwingi kuwatumikia wao lakini hawaridhiki, wananiona kama jalala, wanasubiri nife ndiyo waanze kunisifia, inauma sana pia inakera.”
GPL

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sipendi kiongozi anayeshindwa kutenda haki, ni kukosa uadilifu

    ReplyDelete
  2. Hapo kwanza naona hakuna maelewano hata siku moja zaidi mtaishia kuuza magazeti.wote wanaokimbilia fani hiyo hakuna shule kabisa kwa hiyo ni kijiwe cha majuha.wangalie tangia waanze wapi walikiwa na wanapo elekea zaidi maneno.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad