Nilimsikiliza Mheshimiwa Tundu Lissu na nasikitika kwamba sikubaliani naye jinsi alivyoeleza shutma juu na dhidi ya Mwalimu Julius Nyerere, Baba na Muasisi wa Taifa letu.
Inajulikana na umma wa Watanzania, kwamba mimi binafsi, kama Waziri wa Fedha, nilitofautiana na Mwalimu, nikajiuzulu Uwaziri Decemba,1979, nikimwomba ateuwe Mtanzania mwingine atakayeshauri mambo ya Uchumi na Fedha. Lakini tuliendelea kuwasiliana kwa maelewano bila chuki, na hata aliniteuwa niwe Mwakilishi wa Tanzania na Afrika inayoongea Kiingereza katika IMF (Shirika la Fedha Duniani) chini ya miaka mitatu baadaye Novemba, 1972.
Nimekuwa na mawasiliano na maelewano mazuri sana na Mwalimu hata baada ya kuasisi CHADEMA, Julai 1992 na tulipokamilisha Katiba na Sera za Chadema, nilimtembelea Nyumbani kwake Butiama nikampa azisome ajionee jinsi tulivyonuia kuwahudumia Wananchi wetu. Hata siku moja siwezi kumtusi Muasisi wa Taifa letu. Iwe ni mwiko pia kwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo kumtusi Baba wa Taifa.
Ningewashauri uongozi wa Chadema na hasa Vijana wa M4C (Vuguvugu la Mabadiliko) tuendelee na uhamasishaji : kwa umakini, tukiwa na huruma kwa wanyonge maskini wa kutupwa, tukijiandaa kwa umakini na kiutaalamu Sera na Mikakati ya kuwakomboa toka katika umaskini wa kutupwa kwa kutumia nguvu ya umma (Peoples Power) tukitumia mikakati sahihi: kwani Hakuna Kulala Mpaka Kieleweke:
Mikakati na Sera sahihi ikiwa ni kutumia misingi ya Uchumi na Miundombinu tulionayo licha ya uhalisia dhoofu tulioridhi; tukiwaenzi walioijenga na kuturidhisha kwa unyofu wao.
Roho ya Julius Nyerere ilale mahala pema Peponi. Amen!
With all due respect to Hon. Tindu Lissu, this smacks BAD TASTE.
Edwin Mtei,
Founder Chairman of CHADEMA
Hakumtukana kamwambia ukweli kuwa Nyerere Ni binadamu kwa hiyo kukosea kwa mwanadamu Ni kawaida na anapokosea akosolewe kama alivyokuwa akisifiwa pale anapofanya mazuri
ReplyDeleteAcha mahaba niue! ww Ni kijana acha kuwa na uelewa mdogo km seif Sharif Hamad. Au kwako tusi Ni mpka utukaniwe mama yako? Kamwe na Katu tundu na kizazi Chao chote hawataukaribia uzalendo WA mwl na km ww Ni mfuatiliaji mzuri Mzee Mtei uwa hakurupuki
Deletesawa mnageukana?
ReplyDeleteTundu lisu anausafi gani wa kujilinganisha na nyerere, tundu hana lolote zaid ya ujinga, kukosoa maana yake nn hiv ukimuambia mtu ww ni muongo katili umezoea kuishi kwa uongo hayo sio matusi bali ni nn watanzania tubadilike najua mnapenda sana mabadiliko lakini si kutukana waasis wetu hakuna nchi hata moja inafanya hivo dunian
ReplyDeleteSasa kama kweli asiambiwe tatizo lenu propaganda zimewaathiri Sana nyie na kuwafanya wavivu katika kufikili..
DeleteWATU WAVYOMUAMINI TUNDU LISU SIJUI KAMA NANI KAMA MWALIMU ALIKOSEA KATIKA KIPINDI CHA UHAI WAKE BASI TUNDU LISU ANAKOSEA SASA HIVI HUYU TUNDU LISU MDOMO WAKE UMEJALIWA KUSEMA MANENO MAZURI KAMA NABII WA UONGO AU TAPELI HUWA NAMFATILIA SANA HUTUBA ZAKE ANAONGE MAMBO MAZURI LAKINI HAYAWEZI KUTEKELEZEKA HATA YEYE AWE RAIS KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 KUBWA ATAKACHOFANYA KUJILIMBIKIZIA MALI KAMA WEZAKE NYERERE NA UBAYA WAKE HAJAFIKIA HATUA YA TAIFA LAKE LILOSHIKAMANA KUTAKA KULITIA KATIKA MATATIZO YA KIBAGUZI KAMA HAWA AKINA TUNDU LISU NA CCM YA SASA HUU MUUNGANO WA KISERIKALI ULIKUJA MWISHO KULIKO MUUNGANO WA KIJAMII MUUNGANO WA KISERIKALI UMECHOCHEWA ZAIDI NA MWINGILIANO YA KIJAMII NA MAMBO MENGINE SASA MIAKA 50 IMEFIKA YAANI NUSU KARNE SASA HAWA WANAOHISI MUUNGANO HUU HAUFAI WAKATI UMEDUMU NUSU KARNE BILA KUBAGUANA KATIKA JAMII TUKISIMAMA KAMA VILE SOTE NI WATANZANIA SASA TUNALILIA UTAIFA WA ASILI AMBAO NDIO UTAKUJA KUA NA NGUVU KULIKO HUO UTANZANIA TUTAKE TUSITAKE HUU UTAZANIA NDIO UNAOTUZUIA SISI WANANCHI TUSIBAGUANE KUTOKANA NA IMANI YA SISI NI WAMOJA NA TAIFA LAO MOJA SASA TUNATAKA KUUNDA SERIKALI MPYA MBILI YA TANGANYIKA NA YA SHIRIKISHO MTANGANYIKA ATAKUA UTANGANYIKA WAKE NA MZAZIBAR NA UZANZIBARI WAKE SASA HILI SHIRIKISHO SIJUI NANI ATALIJALI KULIKO UTANGANYIKA NA UZANZIBARI NAHISI HAPA NDO KUTAKUA HAPATOSHI ZAIDI YA SASA KWA SABABU UNAKUA MSHATENGENEZA UPINZANI KATI YA ZANZIBAR NA TANGANYIKA TAIFA LITAENDESHWA KIPINZANI KAMA VYAMA VYA SIASA
ReplyDeleteNyerere ndiye aliyesababisha nchi hii hadi sasa Kila Raisi ajaye anapata kazi kubwa kuiongoza..
Deletewatanganyika tuna tatizo la kutokuwa wakweli kama alivyokuwa Nyerere. Nyerere alikuwa binadamu, kufanya makosa ni ubinadamu. Nyerere hakupenda kunyooshewa kidole wala kukosolewa. Hicho ndicho kimetufikisha hapa. Alidhibiti sana vyombo vya habari,vikaishia kumsifia tu hata alipofanya makosa. Aliposahau kufunga zipu ya suluali yake waliomwambia walikiona , Mtei analijua hilo. Nyerere alifanya mazuri lakini yapo mabaya , kuyasema hayo ni zambi? Mdogo wangu Mtei kizazi cha sasa si cha unafiki wala kusifia uongo, ni PASU KWA PASU. Ukijinyea utaambiwa tu……..
ReplyDeleteGood 1!coment of day!sasa hiv sio zile enzi za zidumu fikra za mwenyekiti hata kama ni pumba!
Deletewatanganyika tuna tatizo la kutokuwa wakweli kama alivyokuwa Nyerere. Nyerere alikuwa binadamu, kufanya makosa ni ubinadamu. Nyerere hakupenda kunyooshewa kidole wala kukosolewa. Hicho ndicho kimetufikisha hapa. Alidhibiti sana vyombo vya habari,vikaishia kumsifia tu hata alipofanya makosa. Aliposahau kufunga zipu ya suluali yake waliomwambia walikiona , Mtei analijua hilo. Nyerere alifanya mazuri lakini yapo mabaya , kuyasema hayo ni zambi? Mdogo wangu Mtei kizazi cha sasa si cha unafiki wala kusifia uongo, ni PASU KWA PASU. Ukijinyea utaambiwa tu……..
ReplyDeletenyerere alikuwa binadam kukosolewa ni jambo la kawaida.
ReplyDeleteTundu lisu ni Msenge anataka kutugawa watanzania aende kule kwao kwa wanyaturu akawagawe mbwiga yeye
ReplyDeleteAnonymous 11:00 AM Acha hayo matusi, toa hoja au pinga kwa hoja. Lisu hakutoa mitusi kama hiyo bali amehoji uongo wa Nyerere. Kama huna hoja kaa kimya. Je? familia yako ikijua kuwa wewe ndo umeandika matusi hayo utaelewekaje?
ReplyDelete