FREEMAN MBOWE AHAHA KUOKOA JAHAZI LA CHADEMA LISIZAME

Mtakumbuka kuwa mara baada ya Bunge la Katiba kuanza, limejitokeza kundi linaloitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA). Malengo ya kundi hili yameelezwa kuwa ni kutetea Rasimu ya Katiba Mpya kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba kwa vile imesheheni mawazo ya wananchi. Vyama vinavyounda umoja huo ni pamoja na CHADEMA, NCCR MAGEUZI, CUF na DP. Kiranja Mkuu katika umoja huu ni CHADEMA chini ya Mwenyekiti Freeman Mbowe.

Ingawa umoja huo umejikita katika kutetea katiba ya wananchi, viongozi wa vyama hivyo wamejinasibu kuendeleza umoja wao nje ya bunge maalum la katiba hususan kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Baraza la Wawakilishi. Katika kucement umoja wao, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza kuwa atavunja Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ili kuweza kuwa accomodate wabunge wa CUF na wa NCCR MAGEUZI. Amesema kuwa hilo litafanyika mara tu baada ya kuanza kwa bunge la bajeti ambalo linatarajiwa kuanza tarehe 6 Mei 2014. Kutokana na maamuzi hayo ya MBOWE, mambo yafuatayo yamebainika.

  1. Mbowe anatangaza kuunda kambi ya upinzani Bungeni kwa kushirikisha vyama vingine katika kipindi ambacho CHADEMA wanakabiliwa na upungufu mkubwa wa wabunge weledi katika kuandaa hoja kinzani na zile zinazowasilishwa na Serikali hasa katika bunge la bajeti. Imebainika kuwa Mawaziri vivuli wengi ni mizigo na ilitangazwa kuwa Mbowe angeteua baraza jipya la mawaziri kivuli kwenye bunge lililopita. Ila kwa vile wabunge wengi waliobaki ni vihiyo, alishindwa kufanya hivyo na sasa anaona umuhimu wa kuwatumia wabunge wa vyama vingine. Kwa ujumla CHADEMA wapo maji shingo katika kuendesha kambi rasmi ya upinzani bungeni
  2. Mbowe ametangaza uamuzi huo mara baada ya mwanasiasa kijana ambaye alikuwa kivutio cha vijana wengi, ZITTO KABWE kuvuliwa madaraka yote ndani ya chama na wapo kwenye mchakato wa kumfukuza uanachama. Imebainika kuwa mara baada ya Zitto kuvuliwa madaraka, vijana wengi wameacha kushabikia chama hicho na kuna wimbi kubwa la vijana kujiunga na chama kipya cha ACT Tanzania ambacho muda si mrefu kitapata usajili wa kudumu. ACT Tanzania imeelezwa kuwa ni mbadala wa CHADEMA na kuna uwezekano mkubwa wa Zitto kuhamia kwenye chama hicho mara tu baada ya kupata usajili wa kudumu. Matokeo ya uchaguzi wa udiwani kwa kata 27 pamoja na uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Kalenga na Chalinze yametoa ishara kuwa CHADEMA sasa kimepoteza mvuto miongoni mwa Watanzania wengi. Hivyo maamuzi ya Mbowe yamekuwa ni ulaghai kwa vyama vingine ili wahisi kuwa wameungana kwa dhati kumbe lengo la Mbowe ni kuokoa jahazi linalozama.
  3. CHADEMA kwa sasa kimepoteza Supporters wengi kutoka dini ya kiislam. Hali imekuwa mbaya zaidi baada ya Zitto Kabwe kuvuliwa vyeo vyote huku viongozi kadhaa wa Mikoa, wilaya, kanda na kata ambao wengi wao ni waislam wakiachia madaraka kwa madai kuwa hawapendwi ndani ya chama chao. Ni baada ya kubaini hilo, ndipo Mbowe alipopiga magoti kwa CUF ambacho kina supporters wengi waislam ili kuokoa jahazi.
  4. CHADEMA kwa sasa hakina mvuto kabisa visiwani ambako CUF ina ahueni. Wakati huo huo, CUF haina kabisa mvuto kwa Tanzania bara huku NCCR MAGEUZI kikiwa ni chama cha Mkoa wa Kigoma tu. hivyo ili kurekebisha majeraha hayo japo vyama hivyo vina tofauti za kisera, vimeamua kuungana kwa muda ili angalau kupata watu wa kuwapigia makofi wanapoenda kuhutubia sehemu ambazo hawakubaliki


Hata hivyo, mnyukano umeanza kujitokeza ndani ya CHADEMA. Baadhi ya Wahafidhina wameapa kutounga mkono maamuzi ya kuwashirikisha wabunge wa CUF na NCCR MAGEUZI. Hoja zinazotolewa ni kwamba kufanya hivyo ni kukizika Rasmi chama hicho. Pia wanasema kuwa vyama hivyo havifanani kisera. Aidha, wanasema kuwa CUF haina wabunge Makini kwenye Bunge la Tanzania ambao wanaweza kuwa sehemu ya Baraza Kivuli. Pia kwa upande wa NCCR MAGEUZI, Wanasema kuwa ukimuondoa David Kafulila ambaye ameweka msimamo wa kutoshirikishwa kwenye Kambi ya Upinzani hasa kutokana na manyanyaso aliyopata akiwa CHADEMA na James Mbatia ambaye amekataa offer ya kuwa Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, kujaza nafasi ya Zitto Kabwe, waliobaki wanatajwa kuwa hawawezi kukidhi matarajio ya CHADEMA. Kutokana na hali hiyo, imeelezwa kuwa Mbowe anahaha ili kuokoa jahazi ndani ya CHADEMA hasa katika kipindi hiki ambacho wapinzani wao, CCM wakiendelea kujiimarisha.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad