IKULU YAMJIBU WARIOBA

Ofisi ya Rais (Ikulu) imesema haikuwatupia virago wajumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu ilitoa taarifa hiyo jana ikirejea taarifa zilizomnukuu aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba akisema: “Ikulu imetutupia virago.”

Jaji Warioba alikaririwa akilalamikia jinsi yeye na makamishna wa tume, walivyoondolewa ofisini na kunyang’anywa magari kwa haraka bila kusubiri siku waliyokuwa wamepanga kufanya makabidhiano.

Taarifa ya Ikulu ilisema kifungu cha 31 (1) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinasema shughuli za tume zinakoma baada ya Mwenyekiti wake kuwasilisha Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalumu la Katiba.

Ilifafanua kuwa Jaji Warioba aliwasilisha Rasimu ya Katiba bungeni Machi 18, 2014 na siku iliyofuata Machi 19, 2014 na kwa mujibu wa Sheria Rais alitia saini tangazo la Serikali kuvunja tume hiyo.

Ilisema tangu mwanzo wajumbe, mwenyekiti, Sekretarieti ya Tume na Watanzania wote waliijua siku ya mwisho ya Tume kukamilisha shughuli zake, hivyo kwa mtu “kujitia ameisahau siku hiyo ni kiwango cha juu sana cha unafiki.”

“Siku hiyo ya mwisho iliwekwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, na Ikulu haikuwa na madaraka wala mamlaka yoyote kubadilisha tarehe hiyo.

Hivyo, madai ya Ikulu kuitupia virago Tume ya Mabadiliko ya Katiba hayana msingi wowote na ni jambo la kutunga tu,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema tangu Tume ilipovunjwa, haikuwa tena na kazi ya kuandaa ripoti au Rasimu kwa sababu kazi hiyo ilikuwa imekwisha.

Kuhusu muda wa kuandika ripoti ya makabidhiano, taarifa hiyo ilihoji kuwa tangu Desemba 30, mwaka jana sekretariati ilikuwa na muda wa siku 77, ilishindwa nini kuiandaa wakati maofisa wake walikuwa wanaendelea kulipwa mshahara na Serikali.

Kurudisha magari

Kuhusu wajumbe kutakiwa kurudisha magari Ikulu, taarifa hiyo imekiri ikitoa sababu kuwa kazi ya tume ilikuwa imemalizika na kwamba magari hayo yanatakiwa kupelekwa kwenye Bunge la Katiba mjini Dodoma.

Hata hivyo Makamu Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Mkuu Mstaafu Augustino Ramadhani na mmoja wa wajumbe, Profesa Mwesiga Baregu wameungana na Jaji Warioba wakieleza kutofurahishwa na jinsi Serikali ilivyowatendea.

Jaji Ramadhani alisema wenzake walipokutana Jumatano iliyopita, yeye alikuwa Arusha na dereva aliyekuwa akimwendesha kwenye gari la tume alimwarifu kuwa gari hilo linatakiwa kurejeshwa, hivyo akamruhusu atekeleze alivyoagizwa.

“Nimeingia Dar es Salaam Jumamosi saa 11:00 jioni, gari nililokuwa natumia lilichukuliwa nikiwa Arusha na niliporejea sasa natumia gari langu mwenyewe,” alisema Jaji Ramadhan.

Kwa upande wake Profesa Baregu alisema hatua zilizochukuliwa na Serikali katika kuvunja tume hiyo zimewafanya wajihisi kama wahaini.

Profesa Baregu alisema, “Heri yetu wengine lakini kwa mzee wetu (Warioba) kutokana na kuwa Waziri Mkuu mstaafu, analindwa na walinzi wanaopata maelekezo kutoka kwa Serikali ambayo imetuondoa kwenye kazi iliyotukabidhi kisheria kama wahalifu, sifahamu hatima yake.”

Alisema Jumatano iliyopita wajumbe wote wa tume walikutana wakakubaliana Ijumaa wakabidhi vifaa mbalimbali yakiwamo magari lakini alipoingia kwenye gari lake kurudi nyumbani, dereva akamfahamisha kuwa wameelekezwa siku inayofuata asubuhi magari yote yapelekwe Ikulu.

Alisema hali ilikuwa mbaya kwa waliokuwa wakiishi na familia zao kwenye nyumba walizokuwa wamepangiwa kwa ajili ya kazi za tume, kwani walitakiwa wazirejeshe mara moja lakini kwa kuwa zilikuwa zimelipiwa mpaka Machi 31 wakaachwa wakabaki mpaka siku hiyo.

Alipoulizwa kama ameitwa Dodoma kutoa ufafanuzi wa Rasimu yao, Profesa Baregu alisema: “Tuliyotendewa tunahisi tunachukuliwa kama wahaini, leo niitwe Dodoma niende kwa imani gani? Sijaitwa na hata ningeitwa nisingeenda.”

Kukabidhi ofisi

Naibu Katibu wa Tume, Kashmir Kyuki alithibitisha jana kuwa makabidhiano kati ya Tume na Serikali yamekamilika.

Kyuki ambaye pia ni Mwandishi Mkuu wa Sheria Tanzania, alisema hata madeni ya Tume yamekabidhiwa kwa Serikali na wameafikiana na Wizara ya Katiba na Sheria itangaze kuwa yapo chini yake, ili kuwaondolea hofu wadai.


Alizungumzia suala la aliyekuwa mjumbe, John Nkolo aliyeugua wakati tume ikiendelea na kazi, alisema pia limekabidhiwa kwa Katiba Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria.

“Tumewaeleza kuwa tuna mgonjwa tuliyekuwa tukimuhudumia, ataendelea kuhudumiwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za ajira serikalini kwa sababu aliugua akitumikia Serikali, watamuhudumia tu,” alisema Kyuki.
Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yeah!! Hiyo ndio liwe fundisho kwa wale wanaofanya vitu nje ya interest ya Nchi na Wananchi. Wakati Nchi nyingine Duniani zinafanya mikakati ya kuungana na kuwa Nchi moja, nyie mnaleta ujinga wa kuigawa Nchi. Hao wanatakiwa wachapwe viboko.

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe anony hapo juu msenge kweli wewe. hivyo unafurahia kitendo walichofanyowa na serikali dhalimu ya babako. muungano lazima uvunjike iwe leo ama kesho haliepukiki hilo. wewe na mafala wenzio mtatukubali tu. IT IS JUST A MATTER OF TIME EVERYTHING WILL COME INTO LIGHT

      Delete
    2. Wewe kweli msenge mwenye ubongo viza! Kwa hiyo ccm na serikali yenu mlitaka tume ichakachue maoni ya wanainchi kwa maslahi ya ccm?
      Nimeamini vibaraka na vikaragosi viko vingi!

      Delete
    3. Wewe kweli msenge mwenye ubongo viza! Kwa hiyo ccm na serikali yenu mlitaka tume ichakachue maoni ya wanainchi kwa maslahi ya ccm?
      Nimeamini vibaraka na vikaragosi viko vingi!

      Delete
  2. UKIVUNJIA WEWE UTAFAIDIKA NINI WACHENI UJINGA NA KUFIKIRIA KUNUNUA GARI PAKUKAA HUNA MAFALA?

    ReplyDelete
  3. Ccm sio wastaabu kabisa, kitendo mlichomfanyia huyu mzee wetu mwenye busara warioba ni udhalilishaji kabisa, kawslisha rasimu vizur mlipoona iko kinyume na matakwa yenu , ndo mnamletea dharau na kashfa, pambafu zenu wote ccm kuanzia mshua hadi mbwa wa mwisho wa chama chenu, hii nchi sio yenu kusema kila kitu lazima mjitengenezee mazingira ya ufisadi mjue kuna kufa, sijui mtajibu nn nyie nguchiro wa kijani

    ReplyDelete
  4. DUH! KIJANI KWELI NOUMA THANA TENA WASENGE WAKUBWA. HIYO RASIMU NI MAONI YETU NA WARIOBA KAYAWASILISHA.MLITAKA ACHAKACHUE?RAIS NAYE UBONGO MDOGO SANA KWA WARIOBA.TENDENI HAKI. MTAUMBUKA TU.TUNATAKA TANGANYIKA YETU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. amewasilisha takwimu za watu laki tatu, hivi tanzania visiwani na bara tuko watu laki tatu shwain wewe ubongo kamasi

      Delete
  5. Kweli jaman ss wananchi ndo tulitaka hivyo kama babu yetu alivyowasilisha hiyo rasimu, sasa nyie mbwa koko wa kijani, mnataka mtoe maoni ya chama chenu badala ya wananchi, huu ni udikteta kabisa, sasa ni kitu gani kilicho wapa nyege mkamsumbua babu yetu kuzunguka hapa tz ili kuleta sera za wananchi alafu mnaziipuzia, na kumdhara kama mtoto, mshua msenge tu mfirwa na obama

    ReplyDelete
    Replies
    1. kuwa makini na mdogo wako, sio kuwa aoymous ukaona hutajulikana unasikia jiangalie

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad