IZZO BUSINESS ALIGOMA KUMPIGIA KAMPENI RIDHIWANI JAPO ALIOMBWA KUFANYA HIVYO

Jumapili iliyopita (April 6), Ridhiwani Kikwete alitangazwa na tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa mshindi wa kiti cha ubungo wa jimbo la Chalinze mkoani Pwani.

Hii ilikuwa habari njema pia kwa Izzo Bizness ambaye aliwahi kumuimbia mbunge huyo ambaye ni mtoto wa Rais Kikwete akimtaka aongee na ‘mshua’ kuhusu hali halisi ya mtaani.

Izzo Bizness ameuambia mtandao wa Bongo5 kuwa tangu atoe wimbo huo amekuwa karibu na Ridhiwani kimawasiliano na hata wakati wa kampenzi za ubunge wa jimbo la Chalinze alimuomba amsaidie lakini alishindwa kufanya hivyo kutokana na hali ilivyokuwa kwa upande wake.

“Kuna vitu vidogo tu ambavyo tulipishana, niliangalia pia katika upande wangu. Hakikuwa kitu cha kusaidiana kimasihala kwa kuwa unapoamua kuingia kwenye kampeni kumsaidia mtu ujue ushaamua kutake risk. Na hapo mimi nilikuwa naenda kukipa tafu chama cha CCM lakini mimi natokea jimbo ambalo limeshikiliwa na CHADEMA na wananchi asilimia kubwa ni CHADEMA”. Amesema Izzo Bizness.

Source: Bongo5
Tags

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dogo sababu zako hazina mashiko, go back to st agrey

    ReplyDelete
  2. Wanaojiingiza kwenye kampeni za siasa wanapoteaga kabisa uliza yupo wapi alipo Malaw sasa hiv

    ReplyDelete
  3. Izo acha uhuni kwan kuish jimbo la chadem kuna usian nn nakaz yako fala kwel aibu yakoo

    ReplyDelete
  4. Bora kaka usipompa kampani ya ufisdi wao hao inzi wa kijani

    ReplyDelete
  5. Izzoo nimekupenda bure unaakili

    ReplyDelete
  6. Unafirwa..shoga nini?

    ReplyDelete
  7. nimekukubali sana izo

    ReplyDelete
  8. izo subiri kampeni ya zito kabwe

    ReplyDelete
  9. Kha ndo nini sasa...we chama gani.....we unataka ushabiki au upo kikazi zaidi?

    ReplyDelete
  10. Hata kama hukupiga mbona kapita, kura yako haijamnyima chochote mh mbunge

    ReplyDelete
  11. Umetumia akili sana maana mwisho wa siku mwenzio anakula bata ikulu na mshua wake wew mbeya city wanakusubir umeona mbal na shoo zako wangeingia vikongwe.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad