JAJI AKATAA MAOMBI YA KUFUTA KESI INAYOMKABILI CHRISS BROWN

Kesi ya Chris Brown itaendelea kuunguruma baada ya jaji Patricia Wynn wa Washington kukataa maombi ya wanasheria wa mwimbaji huyo yaliyomtaka amfutie kesi inayomkabiri.

Mwanasheria wa Chris Brown, Mark Geragos alimuomba jaji afute kesi hiyo kwa madai kuwa waendesha mashitaka walitumia ‘grand jury’ kuuzima ushahidi uliotolewa na mtu ambaye alidai alishambuliwa na Chris Brown na walinzi wake mwezi October, huko Washington.

Jaji huyo alieleza kuwa waendesha mashitaka walikuwa na haki yakutumia ‘grand jury’ kuangalia ukubwa wa kesi yao.

Grand Jury ni huundwa na watu waliopewa mamlaka ya kisheria kupeleleza uzito wa kesi na kuamua kama inapaswa kufunguliwa mashitaka au la, na huwa tofauti na mahakama.

Katika hatua nyingine Jaji huyo ameamua kuwa Chris Brown na mlinzi wake binafsi wasishitakiwe pamoja.

Chris atafikishwa makamani April 17.  

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad