Katika safari ya mapenzi wanandoa huwa wanakutana katika maeneo mbalimbali, wapo wanaokutana vyuoni,shuleni, kwenye nyumba za ibada, sokoni, kwenye daladala, kuunganishwa na mtu mwingine, au baada ya kusikia sauti kwenye simu, redioni, hotelini na sasa wengine kupitia mitandao ya kijamii kama facebook
Ukweli ni kwamba katika mitandao unapoanzisha uhusiano na mtu usiyemfahamu inawezekana ameona picha yako tu nakukuambia kuwa anakupenda na wewe ukiona picha yake ukaridhika naye mkaamua kuanzisha uhusino ni vyema kuonana kabisa ili kuwa na uhakika na uhusiano mnaotaka kuanzisha kwani unahitaji kumfahamu zaidi na ndipo utakapoweza kufanya maamuzi ya kukubali au kukataa.
Anaweza kuwa rafiki yako wa kawaida lakini uhusiano ukaja baada ya kuonana mkafahamiana zaidi, kwani ukikurupuka na kutaka kuoana haraka haraka na yule ambaye mna chat tu kwenye mitandao unaweza kujikuta unajuta baadaye kwa maamuzi yako ni vyema kufahamiana zaidi ya kuchat ili kuwa na uhakika na maamuzi yako....Je Wewe Unaonaje Kuhusu hilo?
INAWEZEKANA,MAPENZI YA KWELI HAYACHAGUI MPENZI UTAMPATA MSIBANI,KWENYE GARI,AU KWENYE MTANDAO,NA HATA MNADANI INATEGEMEA MUNGU KAKUPANGIA WAPI,WENGINE WANAKUTANA HATA BAR.
ReplyDeleteMmh haiwezekani!
ReplyDeleteINAWEZEKANA MIE WANGU NLIKUTANA NA WASSUP
ReplyDeleteon the road to hell da flower can make u happy,,,,,,,,nice way to marry a devil damn!!!!
ReplyDeleteKweli uwezekano upo kabisa
ReplyDeleteKweli kabisa uckurupuke tu chunguza kwanza...........
ReplyDeleteKabla ya kuingia kwenye uhusino lazima kwanza muonane Na hiyo ndo hatua muhimu sana katika hiyo safari
ReplyDeleteNdio maana ndoa za siku hizi ni kama watu wanafanya majaribio
ReplyDelete