KABLA GURUMO HAJAFARIKI ALIMWANDIKIA DIAMOND WIMBO KAMA ZAWADI

Star wa Bongo fleva Diamond Platnumz amesema kuwa siku chache kabla mwanamuziki mkongwe wa muziki wa dansi Maalim Muhidin Gurumo hajaaga dunia alikuwa amemuandikia wimbo kama shukrani kwa kumpa zawadi ya gari mwaka jana.

Diamond alimzawadia mzee Gurumo gari mpya mwaka jana wakati wa uzinduzi wa video yake ya ‘Number 1’.

Platnumz amesema meneja wake Babu Tale alimpa taarifa hiyo njema ya kuandikiwa wimbo na Gurumo lakini kwa bahati mbaya mzee Gurumo alifariki kabla hajamkabidhi wimbo huo.

“Juzi kampigia simu Tale akamwambia kuna nyimbo nimemtengenezea Diamond kwasababu kwa alichonifanyia mimi nimeshukuru sana cha kumlipa mimi sina lakini nimemuandikia nyimbo” amesema Platnumz kupitia 255 ya XXL ya Clouds Fm.

“so alikuwa anamwambia Tale kama ameniandikia nyimbo, so angependa anipatie nikamwambia sawa. Kama siku tatu hivi nyuma, jana ndio nasikia taarifa hizi so najiona kama nimechanganyikiwa hivi.”

Platnumz ameongeza kuwa mara ya mwisho kuonana na Gurumo ilikuwa ni takribani wiki tatu zilizopita baada ya mwimbaji huyo mkongwe kumsurprise kwa kuhudhuria katika show aliyokuwa anatumbuiza Diamond kwa lengo la kutaka kumwona na kumshukuru kwa zawadi ya gari aliyompatia.

“Mara ya mwisho kukutna naye nilikuwa nafanya show Coco akaja maskini ya Mungu mpaka kwenye show…kama wiki moja nyuma kama sikosei au wiki mbili. Akaja akasema nimekuja hapa kukuona, alipenyapenya hadi akaweza kufika pale…nilivyomuona anakuja ilibidi pale nikatishe show nikamsalimia kidogo halafu nikaendelea na show, halafu baadae nikawa niko nae backstage na nini nikazungumza nae.So akasema nimekuja kukushukuru sana sana sana, akasema ningependa uje nyumbani nikamwambia sawa.”Amesema Diamond.

Mwili wa marehemu mzee Gurumo umepelekwa kijijini kwake Masaki, wilaya ya Kisarawe mkoa wa Pwani kwaajili ya mazishi yanayofanyika leo.
Bongo5
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. INNA LILLAH WA INNA LILAH RAJUN, KILA NAFSI ITAONJA MAUTI MUNGU AKULAZE MAHALA PEMA PEPONI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad