KAJALA,WEMA HEBU NISIKILIZENI KIDOGO!

KWENU,Mastaa wa filamu Bongo, Kajala Masanja na Wema Sepetu. Poleni kwa tifu linaloendelea kati yenu. Hongereni kwa kazi za kila siku za kujipatia kipato. Tuweke mambo yote pembeni, mimi kama kaka yenu, hebu tuzungumze kirafiki kidogo leo.

Nimefuatilia kwa karibu ugomvi unaoendelea kati yenu, moyoni imeniuma na nimeona naweza kuwashauri mawili matatu, nanyi mkiona inafaa, muyachukue kama dira ya tatizo lililopo kati yenu.

Kwanza kabisa, kiini cha ugomvi wenyewe mpaka sasa ni kama hakina mashiko. Ugomvi unaendeshwa kwa maneno maneno zaidi ya uhalisia. Nilisikia eti, sababu ya ugomvi wenu ni hii; mlikutana saluni Masaki, Kajala akiwa amelowana kwa jasho kwa vile alitokea mazoezini, Wema alipotaka kumkumbatia, Kajala akakataa kwa nia nzuri ya kutomchafua mwenzake – hapo bifu likaanza.

Inawezekana wakati Kajala akifanya hivyo, alikuwa na nia njema tu, lakini Wema akahisi labda mwenzake anajisikia! Ni kawaida, hatuwezi kufanana mioyo na mawazo.

Tatizo ni pale wanapotokea watu wengine ambao wanakuza huo ugomvi. Kuna watu wanajiita Team Wema, hao nadhani hawana kazi. Wanakesha kwenye mitandao ya kijamii kuchochea huo ugomvi.

Mara inasemwa sijui mmenyang’anyana bwana, mara mmepigana na mengine mengi. Ya nini yote hayo? Kuna wakati hao Team Wema walianza kusema Kajala anatakiwa kurudisha milioni 13 za Wema ambazo alilipa faini mahakamani.
Jamani, thamani ya milioni 13 kwenye matatizo inafanana na kiasi kama hicho kwenye furaha? Siamini kama Wema anazitaka hizo fedha. Alizitoa kwa moyo kwa lengo la kumsaidia rafiki yake.

Niliona picha zilizopigwa mahakamani, wote mlikuwa mnamwagika machozi. Naamini hayakuwa ya kinafiki – ilikuwa furaha. Kwa nini leo mtofautiane kwa jambo dogo? Hata kama ni kubwa, maana inawezekana mna kitu kingine mnachogombania ambacho sikijui, lakini bado nasema kuna kila sababu ya kumaliza hizi tofauti.

Amini msiamini, tofauti zenu hazina maana yoyote. Mtashindwa kufanya mambo makubwa ya maana kwa faida yenu na kubaki mnaendekeza ugomvi ambao mnaweza kuuepuka.

Ninyi ni binadamu, najua mna mioyo, najua kila mmoja anaamini katika imani yake. Uadui umekatazwa kwenye vitabu vyote vitakatifu. Visasi vimezuiwa kabisa kwenye vitabu vyote. Hekima na busara ni sifa njema.

Kusameheana ni kitu kinachoonesha uungwana wa hali ya juu kwa binadamu mkamilifu. Bado mnayo nafasi ya kuzungumza. Hakika nawaambia, mnapoteza mambo mengi ya maana kwa kuendekeza hilo bifu.

Hebu tulieni, vuteni picha wakati Wema unamsaidia mwenzako pale mahakamani, ilikuwaje? Siamini kama ulikuwa unajionyesha kuwa unazo! Sitaki kuamini kuwa una pesa za kuchezea. Bila shaka ulikuwa ni msaada wako kwa kuguswa na matatizo ya mwenzako.

Asitokee mtu akatumia kigezo hicho kuwagombanisha. Huu ugomvi unaweza kuwa na faida kwa watu wengine, siyo ninyi. Mlaanini shetani.
Nawapenda sana dada zangu. Ni furaha yangu kuwaona pamoja tena mkili songesha kwenye tasnia yenu. Ni wakati wenu wa kutafakari! Inawezekana.
Yuleyule,
Mkweli daima,
............................
Joseph Shaluwa

Post a Comment

14 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hivi wale wanaomtetea kajala na kumtukna wema hamuwaon...umeona team wema tu hapo....huo uandishi wako umekaa kinafki tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. mfate kajala umwambie akamuombe msamaha wema yaishe we ukitazama hapo nani wa kuogea, ni kajala, maana yeye kamuibia clement wake kanyamaza, kamsema vibaya kanyamaza nani wa kuombwa msamaha ni wema .

      Delete
    2. Ni kweli kabisa nyinyi wa Pumbav wachache mnaojiita team wema ndio chanzo cha matatizo yote hapa bongo mnatukanisha wasanii mnagombanisha wa2 wasenge kweli nyinyi but nawaambia subirin muda c marefu mtakiona. Na huyo Wema wenu kama hana akil anawaangalia anafikir anapendwa kumbe mnamdhalilisha na yy anaonekana kama nyie tu tatizo shule kuanzia boss wenu mpaka nyie wasenge wenzie

      Delete
    3. Muandishi kaandika vzuri sana mdau hapo juu kataja mnaojiita team wema.kwani nani asiowajua huko mmejazana mamburula na wanaa tu ndiomana mmetajwa nyie.mnakurupuka tu km jengo limeshika Moto sipendi hiyo team makorokocho.nasiwezi kuwa na team zakipumbavu hivi.

      Delete
  2. mungu aingilie kati jamani aya mambo ni makubwa

    ReplyDelete
  3. Clemence kapigwa chini na Wema,kwanza alikua mume wa mtu na Kajala wala hatoki na Clemence mdau umetokota,Wema kugombana ndio zake anakaa na rafiki kwa muda kisha wanagombana tatizo lake ni upeo wake mdogo wa kufikiri,na anafanyavitu kwa kukurupuka na badae anajutia.Maisha mafup. Toeni tofauti zenu maisha ya endelee.

    ReplyDelete
  4. ttz wema anapenda wamuabudu km mungu mtu na ilo kubdi lake feki

    ReplyDelete
  5. Sikien niwambie Wema kama Wema ni mtu mpenda sifa wakati tayali sifa zilisha mlevya sasa kutokufikiria kwake ndo kunaleta matatizo yote haya,kwani nini maana ya mtu kua star? Sitaki kuamini kua star maanake ni kua mtu wa skendo nyingi ambazo hazina hata faida yeyote zaidi ya kukupotezea muda na kukudhalilisha.

    ReplyDelete
  6. Hivi nyie wapumbavu,kila siku story za wema,kajala,lulu,diamond,hamna mada zenye mashiko ?

    ReplyDelete
  7. Team wema kumamayo zenu kwanza mnanuka uchi nyie. Makuma yenu yalokeketwa na mamboro yenu yenye govi, mnagombanisha watu mikundu nyie.

    ReplyDelete
  8. Pata habari mpya kabisa za udaku, skendo na vibwenga kupitia mtandao huu : http://udakuleo.com

    ReplyDelete
  9. Dah'napita njia tu

    ReplyDelete
  10. natamani ningekuwa na namba ya wema na kajala niongee nao kuwapatanisha. Kila mtu alipewa karama duniani, hekema ni moja ya karama zangu. I pray for them wawe na mioyo ya kibinadamu na wayamalize kwani kiukweli LIFE IS VERY SHORT.

    ReplyDelete
  11. BE RICH WITH JUST A VISIT TO THIS WEBSITE
    http://cashnjob.com/index.php?refer=109808

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad