KAMA NI KWELI HUU NI WAKATI WA WAZANZIBARI KUDAI ABDU JUMBE AACHIWE HURU

Hili Bunge la Katiba kwa kweli limefichua Mengi sana hasa kwetu sisi ambao tumezaliwa miaka ya tisini..Nilikuwa sijui kuwa Tanzania kuna mfungwa wa kisiasa. Zipo taarifa kuwa Abdu Jumbe, aliyekuwa raisi wa Zanzibar ni mfungwa akizuiliwa huko Kigamboni na hatakiwi kutoka wala kutembelea Zanzibar kwa kosa la kudai mamlaka kamili ya Zanzibar. 
Kama huu ni ukweli basi huu ni wakati muafaka kwa Wazanzibari wadai kwa namna wanavyoona wao wanafaa uhuru wa mtu wao, aliyekuwa raisi wao na sasa yupo kizuizini nje ya mipaka yao kwa kutetea maslahi ya waliomchagua...
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Replies
    1. Khaaaa we siku zote hujui ndo nchi yako hii ilivyo msema kweli ndo Adui na Mchochezi

      Delete
  2. Ndo manake. Chezea Juliasi wewe.!!

    ReplyDelete
  3. hivi hawa wa znz wanaisaidia nn tanganyika zaidi ya kutunyonya tu kama wanataka znz yao basi waachiwe mpaka wanamfunga baba wa watu kisa kudai uhuru wa nchi yake

    ReplyDelete
  4. Tundu Lisu alisema Nyerere alikuwa muongo na dikteta mkadai katukana.. je? Kumng’oa Jumbe madarakani na kudai eti kajiuzuru siyo uongo huo.. kumfunga kifungo cha nje bila kumpeleka mahalamani siyo udikteta huo.. sijui wabongo tunaumwa ugonjwa gani, kukataa ukweli na kubariki uongo.. au tumelogwa? eeh Mungu tufungue akili zetu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mzee Jumbe baada ya kusaritiwa na wenzake ndani CCM Zanzibar, hakufungwa,ila aligundua ukweli wa siasa kuitwa mchezo mchafu akajipumuzisha Kigamboni.Uamuzi wake uigwe na wazee wenzake wangatuke kukwepa aibu ya kutukanwa na wanasiasa wa kizazi kipya kisichotambu kwanini watanzania tunawaenzi NYERERE na KARUME.

      Delete
  5. kwani yeye jumbe hajui ofisi za amnesty internation mpaka akubali kifungo sio halali? badilikeni nendeni na wakati hizo ni siasa wajinga ndio waliwao sitaki kusikia kitu siasa . kwa wajanja lakini.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad