KAULI YA MBOWE KUHUSU UKAWA KUSUSIA BUNGE

Leo katika kipindi cha KUMEPAMBAZUKA kinachorushwa hewani na kituo cha Radio cha RADIO ONE STERIO nimemsikia Kamanda Aikael Freeman Mbowe akitoa ufafanuzi wa UKAWA kutoka nje ya bunge maalumu la katiba na kutorudi tena bungeni bali kwenda kwa wananchi.

Mheshimiwa Mbowe ameeleza jinsi ambavyo bunge linavyoendeshwa kwa upendeleo mkubwa sana,Matusi makubwa ya nguoni kwa wajumbe wenye mawazo tofauti na ya serikali ya ccm,kutumia vitisho vingi,udhalilishaji na uonevu mkubwa .

Mheshimiwa Mbowe ametolea mfano kwamba Kama Lukuvi amekwenda kanisani na kuanza kuhutubia watu kwamba kama serikali 3 zitapita Jeshi litachukua nchi.Hivi ni vitisho ambavyo kwanza vinampunguzia umakini ama uwezo rais aliyepo madarakani na pia ni kuamsha hisia za jeshi kufanya hivyo hata leo.Kwa maneno mengine ni kuwapa mawazo ama maoni wanajeshi wetu kupindua serikali.

Inashangaza sana Mheshimiwa Lukuvi hawezi kuwajibika kwa kauli hii kwani mwaka 2009 Samson Mwigamba aliwahi kuandika makala fulani kwenye gazeti la TANZANIA DAIMA kuhusu jeshi lakini serikali ya ccm ikamfungulia mashtaka mahakamani kwamba ni mchochezi na analitaka jeshi LIASI TAIFA NA KUFANYA MAPINDUZI ( ARMY MULTINY AND REVOLUTION) na bahati nzuri sana kesi ile Mwigamba alishinda mwezi Fenruary 2014.Je serikali haioni kwamba Lukuvi ameamsha hisia na kufanya uchochezi jeshi kuasi????

Hata hivyo,mimi binafsi nadhani ccm wanakiinimacho wananchi.Wananchi wamesema Wanataka serikali 3 wao wanatoa vitosho vya Muungano kuvunjika,wanatoa vitisho kwamba nchi itaingia vitani,wanatoa vitisho kwamba fanya ufanyalo ni serikali 2 tu na mwingine akasema kwamba hata kama wananchi wanataka serikali 3 basi wasubiri yeye aondoke madarakani kwanza.

HIVI statements kama hizo zinaashiria dalili za nia njema kweli( GOOD POLITICAL WILL) ya kupata katiba mpya kweli???.Nina mashaka makubwa sana kama kweli katiba mpya inaweza kupatikana katika hali hii?
Tags

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. tatizo ni serikali tatu au tatizo ni serikali tatu haina maelezo ya kutosha kuwa ni vipi itafanya kazi hilo ndo tatizo kuwa wanaodai serikali tatu inatakiwa wawe na hoja za kutosha kuwaconvece wananchi ili wakubaliane nao unless otherwise ni propaganda tu kuwa serikali tatu ikipatikana, chadema watashika tanganyika, cuf watashika znz na muungano utashikwa na ccm, hebu semeni hii nchi itaenda wapi?

    ReplyDelete
    Replies
    1. zimwi the ghost face18 April 2014 at 00:07

      We nae mkundu kweli!...kwani serikali tatu si wananchi ndo walipendekeza kwenye ukusanyaji wa maoni? Au kama wanadai watu waliosema hivyo ni wachache kwa nini walitumia hela kuwalipa wale wakusanya maoni??? MATAKO YA MJOMBA AKO!!!!

      Delete
  2. Mshachukua posho mmeona imebaki wiki mnajifanya kwenda kwa wananchi matusi mmeyaona wiki hii hamna jipya

    ReplyDelete
  3. Ukawa mmeishiwa hamana lolote kaz fujo tu

    ReplyDelete
  4. Anguko la ccm litatokea mithili ya mti ulioanguka usiku watu wanaushangaa asubuhi.

    ReplyDelete
  5. Sasa km mtu katishia huko kabisa ni, wee c ukae bungeni uwakilishe waliokutuma.
    Km uamuzi wa serikali tatu au kumi c mpingane kwa hoja na kupiga kura. KUNA JAMBO HAPA.

    ReplyDelete
  6. Huyo anony wa kwanza kachemsha eti unless otherwise huwez tumia maneno yote mawili kw pamoja, c ungeongea kiswahili tu,

    ReplyDelete
  7. Nawashangaa sana hao wanaojihita UKAWA kwa vitendo wanavyofanya, kwanza jwa wale walochafuliwa na Mh. Raisi wa Jamuhuri ni dharau kubwa mbele ya Rais na taifa kwa ujumla sis tunataka nyie mshindane kwa hoja amtaki kushindana kwa hija mnataka kurud kwa wananchi mje mfanye nin kwani hao mua nne waliobaki wanawakilisha viumbe gan? nyie ukawa ndio mnataka kuvuruga amani na kufanya tusgindwe fanya shughuli zetu, katiba inamambo meng rasilimali zetu na hatimaya yake kwa vizazi vihavyo leo mnatoka bungeni jaman mnatuchosha hayo matusi na ubaguz mmeviona leo? vijembe na kashfaa kwa baba wataifa hv vyote mjaviona mbowe tulia tengeneza katiba ni hayo tu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Katiba wanatengeneza wao au ni maoni yanayotoka kwa wananchi!sisi ndio wenyekatiba na maoni yetu ni ya mwisho sasa hao mafisad ma wachumia tumbo wanataka waibadirishe wafanye wanavyotaka wao ili waendelee kutunyonya kwa taarifa yako wew mwenye jina la kike mbele.

      Delete
  8. Naichukia chadema pamoja na viongozi wake hawana lolote kazi uchochezi tu!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Na una wapenda Mafisadi kwa sababu wanatuibia rasilimali zetu na kwenda kuficha kwenye mabenk ya Uswis na wew kuendelea kupata huduma mbovu za afya wao wakienda kutibiwa ulaya sio na wew kusota Kayumba na hali wao wakisomesha watoto wao ulayaaaa!!!!weweeee Mahaba niueeee.

      Delete
  9. I hate chadema, kwani wameishiwa style na mwelekeo pia

    ReplyDelete
  10. nyie ukawa mmekosa sera watu makini hupingana kwa hoja..sasa mnakuja kwetu kutuambia nn kwamba mmeshindwa kututetea au mnatueleza mmechukua kod ndo hz mnafanyia mikutano..kwa upande mwngn nyie ni wanyonyaji wa kod zetu..mmechukua hl kwa kaz ipi?ningekuwa na uwezo kila ambapo mngeitisha mktano mngepigwa mawe...kaz kurubuniwa na wageni

    ReplyDelete
  11. Hongereni Ukawa!!! That's what we call matured politics!!! Tuwakilisheni ipasavyo Watanganyika tunataka serekali yetu na Wazanzibar pia so kuhusu mungano uko pale pale ku pita serekali ya 3 ya Shirikisho!!!! Hili suala la mungano wa serekali 2 ni tatizo tangu zamani!!! Hatujui kilichofanya Karume auliwe kama sio Mgogoro wa serekali 2? Nani anajua hatima ya muuaji lie Hali alijulikana? Big up Ukawa Watz tupopamoja nannying!!!

    ReplyDelete
  12. Mara hati ya muungano, mara serikali tatu saa Hz ibaguzi umezidi bungeni na matusi mbona na nyie hamueleweki au ni kuendelea kupoteza muda muendelee kula hiyo mijihela kwakweli kwa hilo na nyie upinzani mnakwaza sana.

    ReplyDelete
  13. HAWA UKAWA WANASEMA TANZANIAHII NI BATILI CJUI RAI WA WAPI HAWA WANAUKANA URAIA WAO HAWA HAWANA MACHUNGU NA NCHI HII WANASEMA TANZANIA HII NI BATILI SASA WW UNAOWAFATA TAZAMA WALIVYO WAONGO KILA KITU CHAO KINAJITAMBULISHA KAMA WAO TANZANIA NA WAKAPATA UWEZO KUFIKI HAPO WALIPO KWA UTANZANIA WAO WANGEKUA WAKONGO WANGEPATA FURSA HIYO?
    MIMI NAONA HAWA WATU WANA MASLAHI YAO NAWAFANANISHA KAMA WATU AMBAO WANAENDA NCHI ZA NJEE NA KUUKANA URAIA WAO ILI WAPATE KUISHI KWA MASILAHI YAO TAZAMA KIOJA WAO WASHATENGEZA MAISHA KWA JINA LA TANZANIA MPAKA SISI TUKAWAJUA WAO NI NANI SASA WANAUKANA UTANZANIA DUH

    ReplyDelete
  14. Kura ilipipaswa zipigwe kabla ya mchakato wa katiba kujua kama wananchi wanataka muungano au u7baki ujirani.Matokeo yake ndio hayo watu wamepata ulaji laki 5 kwa siku.

    ReplyDelete
  15. Huduma za hospitali za serikali ni mbovu,shule hatuna walimu wa kutosha,hakuna madawati,uchumi ni mbaya,umeme unapanda kila siku,hakuna vitanda vya kutosha mahospitalini,wanyama kama tembo wanauliwa kila kukicha kwa kukosa uongozi bora,na watu wenye uchungu,na nchi yetu ,mimi sijani atoke wapi ila tunatakiwa mabadiliko makubwa,kutoka kwa wananchi ,WANANCHI WA TANZANIA,kwa kuwa ndio wanao umia zaidi,madini yanapita njia za panya,wanachi wengi hawafaidi,elimu ya usalama wa raia na mali zao iko chini,bado watu hawataki mabadiliko?KWELI? asie jua kufa atazame kaburi,?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad