KIKWETE KUVUNJA TUME YA KATIBA LENGO SEREKALI KUUTEKA MCHAKATO WA KATIBA

KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimestushwa na kitendo cha Rais Jakaya Kikwete kuivunja mapema Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kusema haikustahili kuvunjwa wakati Bunge Maalumu la Katiba bado linaendelea.

Kauli hiyo ilitolewa mjini hapa juzi na mjumbe wa Kamati Maalumu ya Katiba kutoka LHRC, Exavery Lwaitama, alipokuwa akitoa mada kwenye warsha ya jukwaa la mchakato wa katiba mpya, ulioandaliwa na Mtandao wa Kufuatilia Sera Mwanza (MPI), na kuwashirikisha viongozi wa asasi na mashirika mbalimbali kutoka wilaya za Ukerewe, Nyamagana, Ilemela, Magu za mkoani Mwanza, pamoja na Wilaya ya Karagwe, Kagera.

Lwaitama ambaye pia ni mhadhiri mwandamizi mstaafu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alisema kuvunjwa kwa tume hiyo wakati Bunge la Katiba halijamalizika, ni kuharibu mwenendo na mchakato mzima wa Watanzania kupata katiba wanayoitaka.

Alisema haiwezekani Rais Kikwete aivunje tume hiyo kisha majukumu yake kuchukuliwa na serikali ambayo tangu awali imekuwa ikikataa kutungwa kwa katiba mpya. “Utavunjaje tume wakati Bunge la Katiba halijaisha? Sasa hii rasimu ya katiba inayojadiliwa bungeni itasimamiwa na nani kama tume imevunjwa? Itawezekanaje isimamiwe na serikali ambayo tangu mwanzo haitaki kutungwa kwa katiba mpya?

“Tunakumbuka mwaka 2011 Mwanasheria Mkuu wa Serikali (Jaji Fredrick Werema), na viongozi wengine wa serikali walikataa kutungwa katiba mpya. Sasa leo rais anaivunja tume, hivi tunategemea kuna upatikanaji wa katiba hapa?” alihoji Lwaitama.

Wakizungumza katika warsha hiyo, viongozi wa mashirika na asasi hizo, walisema hawaoni mwelekeo wa Watanzania kupata katiba mpya wanayoitaka, hivyo wakasema ni bora Bunge hilo likavunjwa, ili kuepusha matumizi mabaya ya fedha.

Mratibu wa MPI, Jonathan Kassim, alisema wameandaa warsha hiyo ili kutoa sauti ya pamoja kwa asasi na mashirika hayo kuhusu mwenendo wa Bunge hilo na kuwaomba wajumbe na serikali kwa ujumla kuwatendea haki wananchi kwa kupitisha maoni yao.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwani walitumwa na nani kutunga hiyo katiba mpya ? Sie wananchi hatujamtuma mtu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kikwete uwezo wake Ni mdogo Sana,,,msimlaum wabaya Ni washauri wake hawana akili pamoja na yeye.

      Delete
  2. Mshua tatizo lake think capacity yake ni ndogo sana, alafu huwa anapenda sana kufanya maamuzi bila kushirikisha watu, pia nahisi huyu alikua hapendi kupatikana kwa katiba mpya ,ili waendelee kujingenezea mazingira ya kufuja mali ya wananchi wa tz, ukwl kwmba huyu mzee sio mtu mzur ndani ya nchi hii

    ReplyDelete
  3. hapa katiba ya nchi hakuna labda katiba ya ccm,..na kwa maoni yangu wajumbe wanaopinga ni bora wajiuzulu kuliko kuambulia kupata ambacho hawajakitaka

    ReplyDelete
  4. Muelekeo ni serekali 3; (1).znzbr (amabayo tayari ipo na katiba yake), (1) tanganyika (itabidi iwepo na itungiwe katiba) (3) ya muungano Tanzania (ibadilishiwe katiba). Na kama haziwezakani basi bora iwe MOJA TU..... TANZANIA, YA MAJIMBO LAKINI.

    ReplyDelete
  5. sheria inasemaje? tatizo sio raisi kulivunja ila sheria inasemaje baada ya rasimu kupelekwa bungeni.
    mzee ameshaanza kuchanganyikwa anashtukaje wakati kila kitu kimefanyika kwa mjibu wa sheria?
    katiba inaweza patikana ingawa binafsi naona ya weza kuwa ya ccm au ya chadema bcoz they are interested in their parties no the country!

    ReplyDelete
  6. Just warch and see what is going to happen!

    ReplyDelete
  7. hakuna katiba hapa ni usanii tu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad