KOCHA MPYA STARS AANZA KWA MIKWALA..AONGEZA WACHEZAJI TISA KIKOSINI

Kocha mpya wa Taifa Stars Mart Nooij ameongeza wachezaji tisa katika kikosi hicho kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki na timu ya Malawi(The Flames) ambayo itakachezwa Mei 4 mwaka huu katika Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Wachezaji walioongezwa ni Edward Charles Manyama (JKT Ruvu),Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hassan Dilunga (Yanga), Hussein Javu (Yanga), John Bocco (Azam), Kelvin Friday (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Nadir Haroub (Yanga) na Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa).
Walioondolewa ni pamoja na beki Kelvin Yondani wa Yanga ambaye aliitwa awali na sababu za kuondolewa ni kushindwa kuripoti kambini,Taifa Stars inategemewa kuingia kambini kesho Aprili 28 jijini Mbeya kujiandaa kwa mechi dhidi ya Malawi.
Wakati huo huo, Tanzania (Taifa Stars) imepangiwa kucheza na Zimbabwe katika raundi ya pili ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.
Kwa timu ya Taifa Stars itaanzia nyumbani ambapo mechi ya kwanza itachezwa kati ya Mei 16 na 18 wakati ile ya marudiano itachezwa Harare kati ya Mei 30 na Juni 1 mwaka huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad