KUFURU:MAPOLISI DUBAI HUTUMIA LAMBORGINI NA FERRARI KUFANYA DORIA

Amini usiamini brand za magari zilizojaa katika garage ya polisi ya Dubai ni Lamborgini, McLaren MP4-12C, Aston Martin, Ferrari, Bentley na Chevrolet.
Source:Bongo5
Mwaka jana tuliwahi kuandika kuhusu chuo cha Dubai ‘American University in Dubai’ chenyewanafunzi wengi wanaomiliki magari ya kifahari duniani, lakini sasa ni polisi wa Dubai ambao wamenunuliwa magari hayo kwaajili ya kufanya patrol za kawaida mitaani.
Dubai-police-cars4
Hata maaskari wenyewe wa Dubai wamekiri kuchanganyikiwa baada ya kupewa magari hayo kwaajili ya kufanyia kazi.
Dubai-police-cars5
Mmoja wa askari hao aitwaye Mariam Ahmed, ambaye binafsi anamiliki Toyota Land Cruiser amesema alipokabidhiwa kuendesha Ferrari FF kwaajili ya doria mitaani hakuamini, na huwa anatamani asipate Off awe kazini muda wote sababu ana enjoy kuwa kwenye Lamborgini awapo zamu.
“Ni mara yangu ya kwanza kuendesha Sport car”, alisema “waliponichagua sikuamini, ni raha sana kuiendesha, nikiwa off huwa naimiss sana siwezi kuifananisha na Land Cruiser yangu”.
Dubai-police-cars7
Aliongeza, “inafurahisha sababu kuna watu huwa wanatuomba tuwakamate kwa sababu yoyote ya kubambikiza ili tu wapande Ferrari wakati wa kwenda polisi”.
Dubai-police-cars8
Askari mwingine aitwaye Abdullah Mohammed , alisema magari hayo yamewaongezea ujiko wanapokuwa wanayaendesha mitaani.
“Kinachofurahisha zaidi katika kuendesha gari kama hiyo ya kifahari ni jinsi watu wanavyokutazama na tabasamu kubwa”.
Dubai-police-cars9
Kwa mujibu wa GeeksTopten Dubai ndio inakamata nafasi ya kwanza katika Top 10 ya nchi zinazoongoza kwa kuwa na magari ya polisi ya gharama zaidi 2014, ‘Top 10 Countries Having Most Expensive Police Cars in 2014’.

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wala sikufuru ndioraha nchi ikiwa namaendeleo Dubai,mchanga dhahabu,maji mafuta unategemea nini?malls zao wanauza wafilipino namataifa mengine wao wenyewe ni ma boss tu.nanchi Yao imeendelea mpk noma,nashangaa huku wakubwa wanakalia kilimo kwanza wakati Barbara zenyewe hakuna,maendeleo hasi hivi hizo kilimokwanza zinaumuhimu gani kuliko maendeleo ya nchi.tuamkee wizi huku umezidi bwana

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwel kabisa hata sis huku viongoz wangekuwa sio walafi na wangekuwa wazalendo mbona ishu ndogo!tuna madin karibu yote tuna mbuga milima maziwa ges sasa hapo jaman tunakosa nin?kazi kuomba tu kila siku!eti tunakopesheka kiongoz anaongea hivyo si aibu hiyi!

      Delete
  2. umesema kweli kaka bongo wizi mtupuuuuuu!!!!

    ReplyDelete
  3. ha ha ha nimecheka basi. sijajua wahalifu ni watu wenye uwezo kiasi gani sasa? manake hata wezi huko kutakuwa hakuna.huko inaonyesha wahalifu ni wale wanaokutwa wakipigana ngumi tu za mtaani.
    utaiba nini ili polisi waseme umeiba. ..biscuit?

    ReplyDelete
  4. wala si uongo viongzi wa tz sio waadilifu hawana uchungu na nchi yao wala wananchi wao, kama wangekuwa hivyo basi hata tz tungekuwa juu sana maana tuna madini, aina zote, tuna bahari mito na milima kwa ajili ya utalii na uvuvi mbuga za wanama and so on haizi haipungui wanajinufaisha wao tu walioko madaraka, ki ukweli katiba hii inahitaji kuwabana viongozi zaidi ili wawajibike kwa nchi yao na si familia zao. inasemekana dubai kuna nyumba kibao za serikali watu wanakaa bure istoshe pia magari yako ya kumwaga kwa bei chee mafuta yanauzwa kama maji safi madukani unategemea nn ni maisha bora kwa kila mdubai, unaambiwa dubai kutembea bila gari ni wewe tu kama unafanya exercise ,amaana unaweza kopeshwa ulipe hata kidogo kidogo kila mwezi mpaka umalize sasa hapo wanafunzi watokosa gari maana bum likiingia anaenda nunua gari lol.

    ReplyDelete
  5. Nimeishi nchi hiyo naipendasana kwakweli nikijahuku naombasiku ziishe nirudi tu Dubai.

    ReplyDelete
  6. The most huge challenge for the Ferrari 430 Scuderia originated from the Porsche 997 GT3, and the Lamborghini Gallardo sports cars. Ferrari execution:
    car dealerships near me

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad