LADY JAY DEE ATOA NAFASI YA MASHABIKI KUHUDHURIA BURE UZINDUZI WA WIMBO WAKE MPYA

Lady Jay Dee anatarajia kuzindua audio na video ya wimbo wake mpya unaoitwa ‘Nasimama’, Jumamosi, April 12. Lakini anahitaji kuwa na mashabiki ambao watapata nafasi ya upendeleo kutokana na kufuatilia hatua zake kimuziki.

Jana, mwimbaji huyo alitoa nafasi kwa mashabiki 15 kushinda nafasi ya kuhudhuria uzinduzi huo bila kiingilio kwa kujibu swali lililouliza Studio ambayo amerekodi ‘Nasimama’ na tayari ilipata majibu sahihi kutoka kwa mashabiki hao kuwa ni Sharobaro Records.

Leo, Anaconda ameongeza swali lingine na nafasi nyingine 15 kupitia akaunti yake ya Facebook na Twitter kwa wale watakaoweza kutaja kampuni aliyofanya nayo video.

“Hii ni kwa walioko Dar es salaam tu, Shughuli inafanyika Nyumbani Lounge Jumamosi April 12.

SWALI: Video ya wimbo Nasimama imetengenezwa na kampuni gani?” Inasomeka sehemu ya maelezo ya Jide.

Kama unataka kuwa sehemu ya uzinduzi huo kupitia nafasi hii maalum, nafasi hii inaweza kuwa yako. Uzinduzi huo utafanyika Nyumbani Lounge.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad