MAAJABU YA MWAKA:MZAZI AMTUPA MWANAWE USIKU ILI ALIWE NA FISI

JESHI la Polisi mkoani Simiyu linamshikilia mkazi mmoja wa kijiji cha Songambele wilayani Maswa mkoani hapa, kwa tuhuma za kutaka kumuua mtoto wake kwa kumtupa na kumtelekeza nje ya nyumba ili aliwe na fisi. Kamanda wa polisi mkoani Simiyu, Charles Mkumbo alisema ofisini kwake mjini hapa jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi majira ya saa nane za usiku wakati mtuhumiwa Baya Seni (30) akiwa amelala na familia yake kijijini hapo, ndipo alipokurupuka ndani akampiga mtoto wake Amos Baya (3) na kisha kumtupa na kumtelekeza nje ya nyumba. Alisema, Seni katika maelezo yake kituo cha polisi alisema alifikia uamuzi huo kwa kuwa hakuona thamani ya mtoto wa kiume kwenye familia yake kwani uzoefu umeonesha kuwa watoto wa kiume wakikua hudai kupata mirathi kutoka kwa wazazi wao . Alisema kinyume chake watoto wa jinsia ya kike wakikua watamuongezea utajiri wa mifugo atakapolipwa mahari ili waolewe na baada ya kuolewa hawawi mzigo tena kwenye familia yake bali mzigo huo huhamia kwenye familia atakayoolewa. Mtoto huyo aliokolewa na majirani baada ya kusikia kilio. Mama wa mtoto huyo Elizabeth Paulo alisema, mume wake alikuwa akimtesa sana mtoto wake akimbagua kwa vile yeye ni wa jinsia ya kiume na kwamba hana faida kwake.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Eeeh jamani baba huyu kweli hajuwi thamani ya mtoto ...Admin tafadhali tujuze matokeo ya badae ya huyu baba tujuwe amechukuliwa hatuwa gani

    ReplyDelete
  2. Crazy ass guy. Wakati wanaume wenziee wanajivunia watoto wa kiume yeye namfanyia unyama. Uyo ni wa kuekwa jela kwa miaka kama kumi akatia adabu. Mtoto ni mtoto haitakiwi kubagua watoto ukiwa kama mzazi hujui atakufaa yupi. Pumbavu zake, kanitia kichefuchefu

    ReplyDelete
    Replies
    1. kufuru za Mungu hizo shwain kweli huyu baba hivi ulimzalia nn

      Delete
  3. Hiyo nayo mpya kumbe cku hiz madem tunamata c mlisema hatuna faida zaid ya kuolewa

    ReplyDelete
  4. Kulikon watu wa kanda ya ziwa mbona mna mambo ya ajabu jaman kwa hiyo mnakosoa uumbaji wake mungu ww baba huna akili kweli yaan unatia kinyaa kny jamii.

    ReplyDelete
  5. aniletee mimi hilo dume ninashida sana na madume

    ReplyDelete
  6. Hilo lizee jinga kweli kaiti na yeye je? Mama yake angemtupa aliwe na fisi? Angekuwepo duniani baada yeye atafute mali anategemea watu waoe ndio apete pesa mimi nimezaa mademu tupu aje achukuwe anipe wanaume

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad