MAGARI YA TOYOTA YAKUTWA NA HITILAFU ..KURUDISHWA JAPAN KUREKEBISHWA

Kampuni ya Toyota Tanzania inatarajia kutoa tangazo ili kufafanua juu ya urejeshwaji magari yaliyobainika kuwa na kasoro za kiufundi.

Hatua hiyo imekuja baada ya kampuni hiyo, yenye makao yake makuu  Japan, kutakiwa kurudisha magari yaliyotengenezwa nchini humo kati ya Januari 2004 hadi Desemba 2010 baada ya kubaini kuwa na matatizo ya kiufundi.

Akizungumza ofisini kwake, mkurugenzi wa Toyota Tanzania, Yusuf Karimjee alisema wanatarajia kutoa matangazo kwa wateja wao yatakayotoa utaratibu wa marekebisho ya magari hayo baada ya kufanya mapitio kwenye takwimu zao na kufahamu ni wateja wangapi nchini watalazimika kurudisha magari  hayo ili yarekebishwe.

“Kama kampuni tunajali usalama wa wateja wetu hivyo kama wenzetu walivyoagizwa hata sisi tunaandaa utaratibu huo,” alisema Karimjee.

Licha ya kutoweka wazi ni magari mangapi yaliyokumbwa na mkasa huo kutokana na kile alichodai ni mapema kuzungumzia hilo, meneja huyo alisema kwa wateja wote ambao magari yao yatatakiwa kufanyiwa marekebisho ya kiufundi, hawatatozwa gharama zozote.

 Kampuni ya Toyota iliagiza magari yapatayo milioni 6.58 kurejeshwa kiwandani nchini humo kwa kuwa usukani (steering), viti na ufungaji wa nyaya za umeme ulikuwa na kasoro.

Top Post Ad

Below Post Ad