MAUAJI YA MZEE KARUME ..ACHA SASA TUHOJI YASIO HOJIKA

The stong man in the world is the one with the best information……..

Hii ni kauli ya waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Benjamin Disarel ambaye aliwahi kutawala kipindi nchi hiyo wakati wa vuguvugu la vyama vya wafanyakazi mwaka 1967, tofauti na watangulizi wake Disarel yeye aliwataka makundi yote ya waingereza wanyonge waliokuwa wanapambana kwa ajili ya maslahi yao kuwa na taarifa sahihi kwa wakati mwafaka hakika haya ni maneno mazito sana.

Naam! Leo tunapoadhimisha Karume Day kuna haja ya kuwa na taarifa sahihi kuhusu kifo cha Mzee Karume ambaye anatajwa kuwa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12 , 1964. Nalisema hili kwa jinsi mambo yanavyofichwa nabashiri kuna uwezekano mkubwa huko mbele tuendako wazungu wakaja kutusaidia kufanya utafiti wa kifo cha shujaa huyo, ili kuelewa nayoyasema rudia makala za mwandishi nguli wa Raia Mwema Bw Joseph Mihangwa au nenda visiwani Zanzibar halafu uliza wakazi wa visiwa hivyo vya karafuu wakwambia sababu za mzee huyo kupigwa risasi mnamo mwaka tarehe7 mwezi wa 4 mwaka 1972? Kisha kwa wingi na mkanganyiko wa majibu ndio utakubaliana nami umefika wakati tuhoji yasiyohojika.

Kwanza swali rahisi hivi ni kweli serikali zetu hizi za Zanzibar na ya Muungano hazifahamu sababu za kifo cha mzee huyo? Hivi ni kweli kabisa mpaka leo tumeshindwa kuweka wazi swala hili? Kwanini? Imefika sehemu tumeruhusu mapambano na malumbano ya wanahistoria kutafiti chanzo cha mauaji hayo ilihali tumeukalia ukweli? Tunaogopa nini? kwa maana tunapojadili mauaji hayo kuna maswali na mtiririko wa kimantiki unaotushawishi kuwa mzizi haswa wa mauaji hayo ni siasa za chuki na kama tunakubaliana katika hili ni lazima twende mbele tujihoji je tumezimaliza hizo siasa za chuki? Au bado zipo?

Hoja ya kwanza katika mtiririko huu ni kuwa kwanza Karume hakuuawa kwa bahati mbaya la hasha! Ilikuwa ni mipango ya watu Fulani na ndio maana ttunasikia matokeo yake ni kuwa baada ya kifo hiko watoto wa mzee huyo walianza kunyimwa fursa zza kimaendeleo kama vile walinyimwa ajira na baadhi yao walifukuzwa kazi haya kayasema mke wa marehemu Karume mama Fatuma Karume akiongea kupitia TBC1 mapema leo, hii ina maana kuwa baada ya kifo hiko chuki haikuisha ikahamia kwa watoto na mke wake ambaye anaweka bayana kuwa ni Nyerere tu aliyewahi kumfariji mama huyo wengine wote walimtoa kwenye kumbukumbu zao hakika hii ni chuki kubwa!

Kutokana na hali hii tunapaswa tujihoji kina nani walihusika na mauaji haya? Na nini kiliwasukuma? Na kwanini chuki hiyo ilifika kwa watoto wake? Je ikiwa bado watoto wa karume wako hai tutaaminije kuwa chuki hiyo imekwisha? Nini mzee karume alifanya mpaka ikatokea hiyo chuki? Lakini tusiishie hapa kwenye mauaji haya kuna jingine , inadaiwa kuwa mzee Karume aliuwawa na mwanajeshi, je kama mwanajeshi ndiye alimwua je hayo siyo mapinduzi ya kijeshi? Kwanini? Lakini pia ingawaje Karume aliuwawa na mwanajeshi cha ajabu ni kuwa uongozi wan chi haukutwaliwa na jeshi bali alipewa mwanasiasa tu Aboud Jumbe!, haya ni maajabu mengine sasa, hivi huyo Hamid aliyemwua mzee karume alitumwa na wanasiasa? Au? Na kama hajatumwa kwanini baada ya mauaji hayo yaliyofanywa na mwanajeshi tunaambiwa kuwa jeshi lilitaka limpe madaraka kanali Seif Bakari hata hivyo baadaye tunaambiwa liliachana na mpango huo, je nini kiliwasukuma kuacha mpango huo? Na nani aliwakataza kufanya hivyo? Hatuoni kuwa iwapo jeshi lingempa uongozi kanali Seif Bakari ambaye pia ni mwanajeshi hatuoni kuwa hayo yangekuwa ni mapinduzi ya kijeshi au uasi wa jeshi? Kwanini jeshi limfanye hivo mzee karume? Aliwakosea nini wapiganaji wake hawa?

Kwa maswali mengi kama haya yasiyo na majibu ndiyo inaibuka haja ya kufahamu je nini sababu za mauaji hayo? Nani alikuwa nyuma ya mauaji hayo? Ni wanajeshi au wanasiasa kwa mgongo wa jeshi? Kina nani hao? Na kwanini? Je chuki zilizopelekea mauaji hayo zilikoma au zingalipo hadi leo? Tukiyajua haya itatuweka huru kwa maana ukweli pekee ndio utatuweka huru vinginevyo tunaficha historia yetu kwa hasara yetu wenyewe! Naam ! wakati ni huu watanzania acha sasa tuhoji yasiyohojika!

...Tafakari!
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wewe wenda mbali sana. Mbona haya mauaji ya hapa karibuni wauwaji wake hawajajulikana mpaka leo hii. Sembuse hayo ya miaka nenda rudi. Kaa ukijua dunia iko ukingoni.

    ReplyDelete
  2. Mimwenyewe ngeni

    ReplyDelete
  3. Duuu haya wadadisi Wa mambo kazi hiyo tunangoja kusoma il I tufahamu siasa zilivyo

    ReplyDelete
  4. Huyo mkewe anaficha aseme tu ukweli huyo karume aliuliwa na shemeji yake i mean kaka yake mkewe

    ReplyDelete
  5. yap hata me niliwah kuckia hivyo ikisha na huy kaka akauliwa na maiti yake kuburuzwa na gari barabarani

    ReplyDelete
  6. Karume aliuawa kwa kulazimisha wazanzibar weusi wajichagulie na kuoa wazanzibar waarabu ili kupata mixer na kuondoa ubaguzi na nyodo za watu weupe. Yeye pia akavuta mtoto wa kiarabu. Shemeji yake ndo kamuua kwa kuchukia dadake kuolewa na mtu mweusi yaani karume sasa. Umeelewa ww mtoa mada. Acha kuchokonoa mambo yaluopita ukishajua ndo itakusaidia nn. Kama chuki ipo inakuhusu nini. The dead are gone. Life inasonga. Kula ugali wako ulale wewe mwenyewe marehem mtarajiwa unahoji kifo cha karume sasa hivi miaka 50 so what! Unless profession yako ni kalam then utakuwa huna akili kabisa . Waache watu wanaokula kwa kuandika upuuzi waandike coz ndo kula yao. Wanaibua mambo ili wauze newz.

    ReplyDelete
  7. nendeni mkafirwe hamjui llote,mauaji ya Karume muulizeni Nyerere na watoto wake Karume na mkishindwa kupata jibu KIYAMA HAKIKO MABLI KWA WENYE AKILI,SIRI ITAJUILIKANA TU.

    NA HAKUNA ASOJUA KUWA KARUME KAUWAWA NA NYERERE, MSHENZI WA MUUNGANO WA GHILBA.

    MWENYE SHAKA NAASEME WAJINGA NYINYI

    ReplyDelete
    Replies
    1. sio mpaka uwaite wajinga waambie kwa kuwaelewesha kwa kuwa ni dhahiri wengi hatujui, sasa ukitukana unakuwa umetuelimisha au umetukosea adabu tu

      Delete
  8. inasemekana alianza kukataa muungano na ndio maana akauwawa chezea nyerere wewe ukileta za kuleta ni bora ufe hehehe mungu amsamehe uko aliko

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad