MSEKWA ATOBO SIRI YA MUUNGANO

Wiki mbili kabla ya Tanzania kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Pius Msekwa ametoboa siri ya Muungano huo akisema “mchakato wa kuundwa kwake ulifanywa kwa siri na haraka sana,” kutokana na upepo wa kisiasa na usalama wa kipindi hicho.

Akizungumza katika moja ya mfululizo wa vipindi vya miaka 50 ya Muungano vinavyorushwa na Redio ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Taifa), Msekwa alisema woga wa hayati Abeid Amani Karume kupinduliwa na maadui, ulikuwa ni miongoni mwa sababu za kuharakisha Muungano huo.

Msekwa aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika wakati Muungano unaasisiwa, alisema pia yeye na wenzake walichelewa kujua kwamba Mwalimu Julius Nyerere (Rais wa Kwanza wa Tanganyika) na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Karume walikuwa na majadiliano ya kuunganisha nchi hizo.

“Kikubwa cha kusema ni kwamba mazungumzo ya Muungano huo yalifanywa kwa siri.... kwa siri sana baina ya waasisi wa nchi hizo. Kwa nini yalifanywa kwa siri? Siyo kwa sababu walikuwa wababe, la hasha, bali kwa mazingira ya wakati ule, kulikuwa na maadui ambao wasingependa nchi hizi kuungana,” alisema Msekwa na kuongeza:

“Kwa woga huohuo, ndipo Mwalimu alipokubaliana na mwenzake wafanye mazungumzo ya siri mpaka waliposaini yale makubaliano na kunijulisha.”

Msekwa ambaye pia amewahi kuwa Spika wa Bunge la Muungano, alisema baada ya makubaliano ya Muungano, Nyerere alimwita na kumjulisha kuwa walishakubaliana (na Karume) kuungana, hivyo walihitaji baraka za Bunge kuridhia Muungano huo.

“Mwalimu akaniambia, ‘wewe Katibu wa Bunge unaweza ukawaita wabunge wakaja kwa harakaharaka kuridhia makubaliano?’

“Nakumbuka siku hiyo ilikuwa Jumanne na Mwalimu alipendekeza wabunge wafike Ijumaa ya juma hilohilo, nao wabunge wakaja wakaridhia.”

Simulizi hii ya Msekwa kuhusu Muungano imekuja wakati kukiwa na vuguvugu la muundo wa Muungano katika Bunge Maalumu la Katiba, kutokana na mapendekezo yaliyomo kwenye Rasimu ya Katiba kupendekeza serikali tatu badala ya Serikali mbili za sasa.

Bunge kuridhia

Aliongeza kuwa, baada ya Bunge la Tanganyika kuridhia Mwalimu Nyerere aliutaka muswada huo “kwa haraka sana”  ili aufanye kuwa sheria na alitaka kupelekewa kwa mkono.

“Baada ya wabunge kuridhia pale Karimjee, nikauchukua muswada na kuupeleka Ikulu, sio mbali pale.

“Mwalimu alifurahi sana, alishajua kuwa ulikuwa umesharidhiwa kwa sababu alikuwa anafuatilia mkutano wa Bunge kupitia redio, ukumbuke zamani hakukuwa na televisheni,” Msekwa anasimulia.

Sababu za kuharakisha

Msekwa alisema kulikuwa na sababu kuu mbili za kuharakisha Muungano; moja ni Mwalimu Nyerere kutaka nguvu ya Afrika itokane na miungano ya nchi, wakati Karume alitaka kuimarisha usalama wa Zanzibar miezi miwili baada ya kuuondoa utawala wa Sultani Januari 12, 1964.

Aliongeza kuwa Nyerere alikuwa amejifunza kutokana na makosa ya awali ambapo maadui waliharibu mpango wa kuziunganisha nchi za Afrika ya Mashariki na kuwa shirikisho.

Hata hivyo, Msekwa aliongeza kuwa, Mwalimu alimwambia Karume wangoje kwa muda, lakini kiongozi huyo wa Zanzibar hakuafikiana na wazo hilo kutokana na masuala yake ya kiusalama.

Alisema hata wakati Bunge la Tanganyika likiridhia muswada wa kuanzisha Muungano, tayari wenzao wa Zanzibar walikuwa wamekwishauridhia.

Muundo wa Muungano

Msekwa alisema suala la kubuni muundo wa Muungano ambalo linasumbua vichwa wajumbe wa Bunge la Katiba sasa, halikuwa tatizo kubwa wakati huo, japo Karume alimwomba Nyerere watengeneze Serikali moja.

“Karume alimtaka Mwalimu waunde serikali moja; yeye awe Makamu wa Rais na Nyerere awe Rais. Lakini Mwalimu hakutaka wazo hilo akihofia maadui wangesema ameimeza Zanzibar na pia alizingatia udogo wa nchi hiyo pamoja na hofu ya kuwa mkoloni mamboleo,” alisimulia Msekwa.

Msekwa alisema mara tu baada ya Nyerere kusaini muswada wa Muungano kuwa sheria, alianza kuunda Serikali ya Jamhuri ya Muungano na aliwachukua wajumbe 20 kutoka Zanzibar kuingia katika Bunge la Muungano.

Alisema baada ya Muungano huo hakukuwa na chokochoko zozote na hata maadui waliotaka kuipindua Serikali ya Zanzibar walikata tamaa.

“Hakukuwa na kitu kinachoitwa kero za Muungano mpaka pale Aboud Jumbe alipoingia madarakani baada ya kifo cha Karume 1972. Jumbe na wenzake walikuwa wanahoji Tanganyika tuliyoungana nayo ipo wapi?” alisema.

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mm haya mambo yananishangaza yupo hai katibu wa baraza la mapinduzi wakati tunaungana kwa nn hamuulizi anaongea msekwa peke yake pili mwaka 1962 mwalim alivikaa vyama vingi kutokana na mazingira ya wakati huo lkn mwalim alivikubali vyama vingi 1992 mazingira ya sasa watanganyika wanataka nchi yao kwa nn hamtaki

    ReplyDelete
    Replies
    1. We msenge poa hayo maswali unamuuliza nani? kamuulize nyerere na karume

      Delete
  2. ww tukana mm ntakujua maana mamlaka ya mawasiliano inazifuatilia number zote zinaotukana mitandaoni na tuna malalamiko mengi ya number yako kutukana sasa ww endelea kutukana

    ReplyDelete
  3. ni dhahiri ssisi hatuna nchi tusiwe wajinga tz ni kwamba na sisi tunataka utanganyika wetu na hatutaki tena muungano ikiwa serikali tatu ni zolotesha muungano kwanini basi muungano usife na tuwe huru na lawama ziishe shwain

    ReplyDelete
  4. mmh 2muachie mungu.

    ReplyDelete
  5. mmh mbona wabongo 2napenda 2kana badala ya kujibu hoja za msing 2taendelea mpaka lin wandugu 2badilike.

    ReplyDelete
  6. Msamehe hiyo anayetukana!watu hatufanani.hoja mbele yetu mzuri engine wanatukana,wacha watu waseme ili tuelimike.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad