MTIKILA "WAKATI WA KUDANGANYANA KUHUSU MUUNGANO SASA UMEKWISHA"

Mjumbe  wa Bunge Maalum la Katiba, Mchungaji Christopher Mtikila, amesema kuwa hivi sasa ndiyo muda mwafaka wa Watanzania kuambiana ukweli kuhusu Muungano. Mchungaji Mtikila (pichani) alitoa kauli hiyo bungeni jana alipoomba mwongozo wa Mwenyekiti wa Bunge hilo Samuel Sitta, baada ya mjumbe Tundu Lissu, kutoa ufafanuzi wa wa maoni ya wajumbe wachache wa Kamati namba 4.

Mchungaji Mtikila baada ya kuruhusiwa kuzungumza, alisema alisema kuwa kwa zaidi ya miaka 50 Watanzania hawajawahi kuambiwa ukweli kuhusu Muungano na kusema kwamba badala yake wamekuwa wakiambiwa uongo na kwamba ndiyo maana Mungu hakuibariki Tanzania kwa kipindi hicho chote.

“Tulijengwa katika uongo na ndiyo maana Mungu hakutubariki kwa miaka 50,” alisema Mchungaji Mtikila.

Mchungaji Mtikila akijibu kauli ya Peter Serukamba, aliyehoji kuwa wajumbe hao wapo bungeni hapo kama nani kama Muungano hauna uhalali kama alivyosema Lissu, alisema:

Ndiyo maana tumekuja kufanya kazi ya kutengeneza Katiba na kuandika upya historia.”

Mchungaji Mtikila alisema kwamba hivi sasa Tanzania ina watu milioni 45 na kwamba hakuna sababu ya kuendelea kuwaeleza uongo kuhusu historia ya Muungano.

Mchungaji Mtikila ambaye kwa miaka mingi amekuwa akiupinga Muungano, alisema kuwa kinachotakiwa kwa sasa ni kuambiana ukweli.

Aliongeza kuwa Watanganyika wanahitaji kuwa na haki ya kupata serikali yao pamoja na Wazanzibari kujitambua na kuwa na taifa lao.
CHANZO: NIPASHE
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli kabisa mzee wangu

    ReplyDelete
  2. Tuna matatizo mengi yanayotukabili na lazima tukubali ukweli kuwa kabla ya hilo bunge wananchi ndio ilikuwa waamue kwa kura ya maoni kama tuendelee na muungano au hapana.As simple as that baada ya hapo ndio tujadili mengine.Swala la muungano sio la kuijadiliwa na watu wachache ambao wana agenda zao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Aisee ni kwel kabisa haiwezekan tukapangiwa mambo na mafisad wala nchi ambao kwa miakaa yote hii wanatubuluza tu!huu nduo muda wakuwaumbua mafisaf na kuikomboa Tanganyika yetu!

      Delete
  3. Mtikils ni jembe,aliwahi kusema hivii,"Tanganyika ni mama yetu,kushabikia muungano ni sawa na mtu mwehu anayeshangilia, mama yake akibakwa'

    ReplyDelete
    Replies
    1. umeona ee mtikila kaongea jambo jema, tunahitaji tanganyika yetu znz tayari wana serikali yao, sisi tuko wapi hata kisheria hatutambuliki tumejigubika katika muungano but hatujulikani tuko wapi

      Delete
  4. Mmh, nchii tukigawana watakaozidi kunufaika ni walewale wachache tu,

    ReplyDelete
  5. ww babu unazeeka vibaya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad