MWALIMU NCHINI KENYA AMCHAPA FIMBO MWANAFUNZI MPAKA KUFARIKI

Hii ni taarifa kutoka Kenya ambapo inasemekana Wazazi katika kaunti ya Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya mwalimu mmoja kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi kupoteza maisha.
Mtoto huyo inasemekana alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai na alipokua akipelekwa hospitali alifariki dunia,ambapo wazazi hao wameandamana kwa amani wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
Polisi nchini Kenya wamemtia mbaroni tayari mwalimu huyo na kwa sasa anashirikiwa na Polisi huku uchunguzi zaidi ukiendelea kufanywa,Mtoto huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi iitwayo Roka Preparatory.
Wengi wa wazazi wenye watoto wao katika shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule nyingine ambapo Nchi ya Kenya iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi iliyopita na hii ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na kuwajeruhi kukithiri.
Source:Bbc Swahili.

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huyo mwalimu akatupwe gerezan huko, mshenzi sana, alafu pia kamuaribia huyo mwenye shule, kama wazazi ndo watafanya kweli kuuwamisha watoto wao kwnye hiyo shule, huyo mwenye shule si atakufa njaa jaman

    ReplyDelete
  2. Walimu wengi kwenye shule za private hawajasomea ualimu,hivyo maadili hawana,hata hapa kwetu wengi tu na hii ndo maana elimu inazidi kushuka.

    ReplyDelete
  3. Afirwe azae na yeye

    ReplyDelete
  4. Auwawe mbona yeye kaua.

    ReplyDelete
  5. hii picha mliyotumia inaonyesha a pervet,mbona mwalimu wa kiume kumpiga msichana kwenya makalio,anania gani

    ReplyDelete
  6. kabla hajafungwa mleten nimfire uyoo

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad