Akizungumza jana, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema viongozi wa Ukawa ni genge la wasaka madaraka hivyo hawawezi kuungana kwa hilo.
Nnauye alisema viongozi wa vyama vya upinzani waliungana kwa lengo la kutafuta Katiba bora, lakini wamebadilisha ajenda na sasa wanazungumzia urais mwaka 2015.
“Hawa kumbe ni waongo, malengo yao siyo Katiba, bali ni kutafuta madaraka, muungano wa kutafuta madaraka hauwezi kufanikiwa kwa sababu viongozi wote wa Ukawa ni wapenda madaraka,” alisema Nnauye.
Alisema wananchi watashuhudia umoja huo ukisambaratika kwa sababu viongozi wa Ukawa hawawezi kuvumiliana na kuachiana madaraka.
“Kuungana ni jambo zuri, lakini sababu za kuungana zinapotajwa kuwa ni kumsimamisha mgombea mmoja wa urais mwaka 2015, watasambaratika kabla ya muda huo kufika,” alisema.
Alisema Ukawa wamewadanganya wananchi kwamba wanasimamia Katiba bora kumbe ajenda kuu ni kuongoza nchi.
Gazeti hili jana liliripoti kuwa Ukawa pia wanataka kusimamisha mgombea mmoja wa ubunge katika kila jimbo la uchaguzi.
Katika habari hiyo, Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba na Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia walikiri kuwapo mpango huo.
Taarifa za kuwapo mpango, zimekuja siku chache tangu kufichuliwa kwa mpango mwingine wa kuundwa upya kwa Baraza la Mawaziri Kivuli ambalo litawajumuisha wabunge wa vyama vya upinzani katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano wa bajeti unaoanza Mei 6, mwaka huu.
Nape mpuuzi tu hajui anachosema
ReplyDeletempuzi wewe unaeingia kizani bila kujijua
DeleteNa wew unaedhulumiwa na mafisadi vip hujapotea kutetea majizi n machumia tumbo huoni hapo umezikwa kama sio kupotea?tafakari wewe mtoto wa fundi bomba.
Deletempuuzi wewe usielewa anachosema
ReplyDeleteMnataka kuwadhulumu wananchi,mmewadhulumu haki ya kuchagua kama muungano uwepo au la,sasa mnapiga propaganda nyingine,chukueni posho msione aibu!
ReplyDeleteHuyu CHOKO naye anaonfea pumba gani?katetee mafisadi kuma wewe.
ReplyDelete