Rai yangu kwenu wanaume wenzangu...
Waheshimuni sana WANAWAKE.
Nimegundua kwamba kumdharau mwanamke yoyote yule ni sawa na kumdharau mama yako mzazi kwasababu mama yako nae alikua binti wa kawaida tu kabla hajakuzaa wewe.
Vivyo hivyo huyo mwanamke unayemdharau leo will probably be mama wa FULANI in the near future.
Huyo FULANI anaweza akawa Rais wako, mchungaji wako n.k, bila kujali kwamba amezaliwa(ametoka) kwenye tumbo la mwanamke wa aina gani (malaya au anayejiheshimu). Kitanda hakizai haramu.
Nina ushuhuda...
Dada yangu amejifungua, nilikua nasikiaga tu eti "hakuna kama mama", sasa nimethibitisha.
Hakubahatika kujifungua kwa njia salama, hivyo baada ya kujifungua ameteseka sana na mshono, wakati huohuo halali usiku, mtoto akihitaji kunyonya hata kama ni usiku wa manane anaamka kwa tabu kwasababu ya maumivu makali ya mshono anayoyapata, ila anahakikisha anamnyonyesha au kumbembeleza.
Wakati mwingine mtoto akicharuka halali usiku kucha, namuonea huruma sana ila yeye kwake ni faraja kumuona mwanae kapumzika!
Imefikia kipindi namtazama mama yangu usoni bila kummaliza, kumbe alipata shida zote hizi!
NAWAHESHIMU SANA WANAWAKE WOTE! Maneno haya yanatoka moyoni mwangu.
Ni kweli jamani...hata katika maisha ukimdharau mama maisha yako hayatakuwa na aman kamwe. Wanawake ni watu muhimu sana duniani...huruma,upendo na mengine mengi...
ReplyDeleteJamani mimwenyewe hapa nilijifunguwa kwa operation myaka miwili iliyopita ila hadi leo ayo maumivu nayakumbuka... Sisi wanawake ni watu muhimu sana na uchungu wa mwana aujuwa mama yake
ReplyDeletehakuna kama mama!nakupenda sana mama yangu
ReplyDeleteMwanamke ni mtu mhimu! Asiemdhamin hana maana
ReplyDeleteJaman sio kuzaa Tu Mimi hapa Nina ujauzito na unanitesa yaan siwez Kula wala kulala nateseka hadi najiona Nina nn dunian hapa yote haya natamani Tu kuitwa mama
ReplyDelete