SITTA"KUANZIA SASA TBC1 WAKIKATA MATANGAZO HATUWEZI KUKATISHA KUENDELEA NA BUNGE"

Jumamosi iliyopita matangazo ya Television ya taifa yalikatika wakati ikiwa live kwenye bunge la katiba ambapo Mh. Tundu Lissu alikua akiwasilisha maoni ya wachache ambako kulisababisha Mwenyekiti kuahirisha bunge hilo mara moja baada ya kugundulika hawakuwa wanaonekana live.
Kukatika huko kwa matangazo ambako badae kulitangazwa kwamba ni kutokana na hali ya hewa kulifanya TBC itupiwe lawama au malalamiko yakiwemo kutoka kwa baadhi ya viongozi na Wananchi huku baraza la habari likisema ni kitendo cha aibu na watafatilia kujua kama ni kweli hali ya hewa au hujuma.
Baada ya hayo yote na kauli zilizotolewa na Wanasiasa mbalimbali baadae, Samwel Sitta ambae ni Mwenyekiti wa bunge la katiba hapa 104.4 Dodoma ametoa taarifa rasmi akisema >> ‘kuanzia sasa matangazo ya live bungeni TBC1 yakikatika hatutawezi kukatisha kuendelea na bunge’
‘Tunazingatia kwamba ipo Radio na Wananchi wengi wa Tanzania wanasikiliza radio na mtu mwenye TV hawezi kushindwa kununua radio kwa hiyo hatuwezi kukatiza kila wakati, ikiwa radio inaendelea kazi yetu humu ndani itaendelea’ – Samwel Sitta
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Huwezi amini nimeumizwa sana na kauli hiyo na imenisikitisha sana mim huku nilipo Meatu hakuna radio stesheni yoyote inayo patikana mpaka tv kwakua tunategemea kebo sasa kwa maamuzi hyo nikutukosesha haki yangu ya msingi ya kidemokrasia kama mwananchi wa nchi hii...

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad