SITTA:SAINI ZA NYERERE NA MSEKWA ZIMECHEZEWA KWENYE HATI YA MUUNGANO

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta amekiri “kuchezewa” kwa saini ya hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na sehemu ya saini ya aliyekuwa Katibu wa Bunge la Tanganyika, Pius Msekwa zilizopo kwenye hati ya sheria ya kuridhia Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Akizungumza na gazeti hili jana, Sitta alisema ni kweli kuna maneno katika hati hiyo ya sheria namba 22 ya 1964, iliyosainiwa na Nyerere na Msekwa, Aprili 25, 1964, yameongezwa.

Alisema katika saini ya Nyerere kumeongezwa herufi “us” kwa kompyuta na katika sehemu ya saini ya Msekwa kumeandikwa neno “Msekwa” kwa kompyuta, jambo ambalo ni makosa. Sitta alisema walioongeza maneno hayo ni wafanyakazi wa ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali baada ya kuona sehemu ya maandishi kwenye saini hizo hayasomeki, lakini walifanya makosa.

“Wale vijana walipoona document (nyaraka) haisomeki waliongeza “us” mwisho kwa kompyuta kwenye saini ya Nyerere, ila walifanya makosa maana bora kitu kionekane kufifia hivyo hivyo lakini kibaki na maana yake,” alisema.

Hata hivyo, Sitta alisema kwa waliofanya kazi na hayati Baba wa Taifa wanatambua saini iliyopo kwenye hati ya sheria hiyo ipo sawa ukiondoa makosa ya kuwekwa herufi hizo.

Kuhusu saini ya Msekwa, alisema pia kulifanyika makosa katika sehemu ya saini hiyo, kuandikwa kwa kompyuta “Msekwa”.

“Ni saini ya Msekwa, lakini vijana wa chamber kwa AG waliongeza neno “Msekwa” kwa kompyuta. Ni mtu asiyejua thamani na uhalisia wa saini ni kubaki ilivyo hata kama kwa miaka 100 hata mtu aje kuisoma kwa darubini,” alisema.

Hata hivyo, alisema maudhui ya hati ya sheria hiyo, iliyosainiwa rasmi Aprili 25, 1964 ni sahihi kama ambavyo walikubaliana waasisi wa Muungano, Nyerere na Karume.

Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema alisema kwamba hafahamu kama ofisi yake inahusika na kuchezewa kwa saini hizo, tofauti na madai ya Sitta.

Sheria iliyopitishwa Z’bar

Sitta alisema ili kuondoa utata, ameagiza kupatiwa hati ya Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Abeid Karume (Presidential Decree) aliyotoa kusaini makubaliano kwani wakati huo, hakukuwa na Bunge.

“Karume alitumia Baraza la Mapinduzi akatumia amri ya Rais akasaini. Tunatarajia kuipata hiyo, sasa tutakuwa tumepata nyaraka za Bara na Zanzibar,” alisema Sitta.
Tags

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. mnatuzingua, wapeni wazenj nchi yao... Acheni kung'ang'ania maana hawafaidiki na muungano toka uanzishwe

    ReplyDelete
    Replies
    1. hata na sisi hatufaidiki nao hasara tu wanatupa kuwagawia gawia ruzuku

      Delete
  2. Kijana hapo juu tengua kauli yako, wazenji sio kama hawanufaiki na muungano, tunaotakiwa kulalamika ni ss wa tanganyika, kwasababu sijasikia mtanganyika yoyote ambayo anaishi zenji alafu akawa huru kabisa na mambo yake kama wao wa zenji wanavyooenjoy uku kwetu tanganyika, hvyo muungano uvunjwe na wa zenji wote rudini kwenu, mnanyodo sana huko kwenu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mavi ww.wacha kuongea pumba.na ww rudi kwenu kishumundu

      Delete
  3. Mimi nashangaa kama Tanganyika muungano kero kwetu si tuwape nchi yao wakifanya vizuri wakifanya vibaya shauri yao.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ila kuna kitu inaonekana bara wananufaika na muungano why wameung'ang'ania? wa zanzibar hawataki niwaz hawanufaiki.kweli bwana wawaachie nchi yao wakishindwa watajijua c ni wao?!?

      Delete
  4. Muungano ukivunjwa wapemba wote rudini kwenu hatuwaki hapa kwetu, mnadharau sana nyie viumbe vya ajabu

    ReplyDelete
  5. Kwenu wapi? DRC

    ReplyDelete
  6. Inawezekana watu wengi hawana uelewa na muungano,kinachotakiwa ni kutatua kero za muungano,kuvunja muungano siyo kutatua,halafu kinachoongelewa hapo ni kughushi sahihi ya mwalimu kwenye hati ya muungano,issue ya muungano ningewashauri viongozi suala hili waliweke wazi lizungumzwe kwa mapana hasa zanzibar cuf na ccm wakae kwa pamoja wakubaliane wanataka muungano Wa aina gani ndo wake Tanzania,ili wasiwachanganye wahanchi,ukiangalia cuf wanataka serikali tatu,ccm serikali mbili wote zanzibar,wakati huo waziri wa sheria kwa zanzabar anatoka cuf,viongoz achen tamaa ,wahusishen wananchi waseme wanataka muungano gani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sahihi zote zipo sawa tttzo lililokuwepo ni nyongeza ya maneno "us" na "msekwa" ambayo yalikua yamefifia. Safi Sana kwa ushauri Wako WA muungano

      Delete
  7. Mm naona kama muungano ni muhimu bac tuwe na serikali moja ikishindikana bac Tatu na sio mbili.

    ReplyDelete
  8. Me kwa uwelewa wangu jinsi ninavyoona hapo muungano unawafaidisha viongozi wachache WA CCM na sio watanzania

    ReplyDelete
  9. achani usenge nyie machogo kama vp na nyinyi rudini mikoan kwen maana cost area yte ya wazanzibar mumeipora tu na wazungu wenu

    ReplyDelete
  10. Zanziber ikiachiwa huru lazima watapigana vita vya wenyewe kwa wenyewe maana waharabu hawana mana hata kidogo

    ReplyDelete
  11. waharabu?Duh!Kiswahl tatzo na janga kubwa

    ReplyDelete
  12. MUUNGANO HAUNA FAIDA KWA WAPINZANI KWA SABABU NDIO UNAOWANYIMA MADARAKA NDIO MAANA KELELE NYINGI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad