Kutokana na mvua zinazonyesha hivi sasa kwenye jiji la Dar es salaam pamoja na kusababisha mambo mengi kusimama, miundombinu kuharibika hasa madaraja yanayounganisha njia kuu, pia zimesababisha vifo vya watu 10.
Nyumba nyingi zimeingia maji hasa maeneo ya mabondeni na kulazimisha familia kuhama kutoka kwenye makazi yao ambapo mpaka sasa Polisi Dar es salaam inasema watu kumi waliofariki, wamo watoto watano na watu wazima watano.
Kamanda Suleiman Kova wa kanda maalum ya Dar es salaam amesisitiza hali sio nzuri hivyo wananchi wanatakiwa wachuke tahadhari kwenye makazi yao na hata wanaotembea na magari barabarani kwa sababu njia nyingi zina mashimo na pia watu wapunguze mizunguko isiyo lazima barabarani.
TAARIFA YA POLISI KUHUSU IDADI YA WATU WALIOFARIKI KUTOKANA NA MAFURIKO
April 13, 2014
Tags