TIMU YA WATOTO WA MITAANI YA TANZANIA YACHUKUA KUMBE LA DUNIA

Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania jana April 06 imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada kuifunga Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro Brazil.
Mshambuliaji Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi kwenye mechi hiyo akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza George Osborne.
Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0,Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.
Timu ya Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nyie mamburura ikuzeni hiyo timu iendelee kututoa ktk matope.badilikeni acheni wizi,siasa endelezeni mchezo wa soka.HONGERENI SANA VIJANA.

    ReplyDelete
  2. hongereni watoto yaaan lini za wakubwa zitatusua bas tujitahid kukuza hawa

    ReplyDelete
  3. Safi ndg zetu, ila sasa muwalipe vizur ili wawe na moyo wa kujituma zaidi, isiwe kujituma kwa watoto nyie ndo mnatunisha matumbo yenu na kusomesha watoto wenu kwnye shule za kifahar, tanzania tuamke jamani roho za ubinafsi tuache

    ReplyDelete
  4. kwakua tanzania hatuna mipango hiyo timu itaishia kusambaratika kama ilivyokua kwa vijana wadogo waliopita kama serengeti boys.

    ReplyDelete
  5. Wamenifurahisha

    ReplyDelete
  6. Ongeleni wanangu, Serikali musiwadhurumu hawa watoto jamani kaa zambi zitawapeleka motoni

    ReplyDelete
  7. Itabidi na ya wakubwa wachukuliwe wa mitaani maana wameonesha wana uzalendo

    ReplyDelete
  8. Ni kweli naafiki mawazo ya wote hapo juu lakini sina imani na walengwa wakisha anza kuwasaidia basi timu inakufa maana watawapeleka watoto wao wasiojua kucheza wajidai ndio watoto wa mitaani hapo roho zinawauma kweli kwa nini hawakuwapeleka watoto wao. hii ndio bongo ninawasiwasi hata hao wanariadha wanaotakiwa wakafanye mazoezi nje ya nchi kama watakwenda wahusika kweli maana wamezoea kutupelekea jamaa zao wakafanye shoping wahusika wanaachwa wakilalamika bila kusikilizwa na yeyote

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad