Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imefanikiwa kuingia fainali za mashindano ya Kombe la Dunia la Watoto wa Mitaani baada ya kuifunga Marekani goli 6-1 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali uliochezwa jana (Aprili 5 mwaka huu) jijini Rio de Janeiro Brazil.
Mpaka timu zinaenda mapumziko Tanzania ilikuwa mbele kwa goli 4-0,goli pekee la Marekani katika mchezo huo ambayo hadi nusu fainali ilikuwa haijafungwa lilifungwa dakika za mwisho za mchezo huo.
Kwa matokeo haya Tanzania inacheza nusu fainali na Burundi,Mechi hiyo inachezwa leo (Aprili 6 mwaka huu) ambapo Burundi imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Pakistan goli 4-3 katika nusu fainali ya pili.
Mchezo huo wa fainali unachezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense katikati ya Jiji la Rio de Janeiro huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza George Osborne.
Katika mechi ya kwanza katika kundi B la michuano hiyo,Tanzania ilicheza na Burundi na kutoka sare ya mabao 2-2.
go Tanzania,goo........!
ReplyDeleteTaifa stars ya kesho
ReplyDeleteWanasitairi sifa sana inabidi watunzwe waje watufaye baadaye
ReplyDeleteTuambie habari za uhakika wameingia fainali au nusu fainali mbona unashindwa kupangilia maneno kichwa cha habari kinasema fainali na habari yenyewe ndani inasema nusu fainali na Burundi nyoosha maelezo..
ReplyDeleteYn hata haeleweki,mara fainali mara nusu fainali,hizo ndo faida za kucopy n paste,uwe unahakiki kwnza hbr kabla hujarusha hewani,idiot!
ReplyDeleteLiadmin lifala kinomanomau
ReplyDelete