Wakati Rais Jakaya Kikwete akitarajiwa kuhutubia wafanyakazi katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), limeitaka Serikali kupandisha kima cha chini hadi kufikia Sh750,000.
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicolas Mgaya alisema jana kuwa wanahitaji kuona wafanyakazi wakipata kiwango cha mshahara kinachokidhi mahitaji.
Alisema kutokana na kushuka kwa thamani ya shilingi na mfumuko mkubwa wa bei uliopo kwa sasa, kiwango hicho angalau kinaweza kukidhi mahitaji muhimu ya wafanyakazi wa kima cha chini, ikiwamo malazi, mavazi, chakula na mahitaji ya afya.
“Katika hali halisi, tunaona namna bei za vitu muhimu ikiwamo umeme, maji, mafuta, gharama za vifaa vya ujenzi, nyumba vyakula na gharama nyingine za maisha zimekuwa zikipanda maradufu katika miaka ya karibuni, lakini hakuna namna inayofanyika kuleta unafuu kwa wafanyakazi.
Kimsingi kima cha chini lazima kiongezwe ili kikidhi mahitaji ya maisha ya wakati huu,” alisema.
Word
ReplyDeleteMhh,never in this country!
ReplyDeletejamani iwe hvyo tu khaaa hii mishahara waupata cku hyo hyo unaisha yaan
ReplyDeleteHizo ni hadithi tuu hakuna kitakacho fanyika hapo huo ni uwizi mtupu wanashiba wenyewe sisi hali ya chini hakuna kitu tutakachopata hapooo
ReplyDelete