UKAWA"HATUJAMPIGIA MAGOTI ZITTO KABWE"

Habari inayoenezwa kuwa viongozi wakuu wa UKAWA na hata waandamizi nikiwemo mimi, eti tumembembeleza mhe. Zitto Kabwe ili aunge mkono mikutano ya UKAWA kuzunguka nchi siyo taarifa zenye ukweli wowote.
Mhe Zitto hajawahi kufuatwa na viongozi kuombwa ashiriki ktk shughuli za UKAWA. Na hadi sasa UKAWA haijatangaza shuguli zozote zile zaidi ya mkutano wa Zanzibar ambao pia polisi wamekataa usifanyike leo hadi mara nyingine.
Kwa bahati nzuri, wakati mhe. Zitto Z Kabwe akichangia sura ya 1 na ya 6 bungeni, alionesha njia sahihi kwa taifa na kwa asilimia mia moja aliunga mkono hoja za wananchi na hata mapendekezo ya UKAWA.....Kwa mfano Zitto Kabwe alisema, "hoja ya serikali tatu kuvunja muungano siyo ya kweli. Alisisitiza kuwa muungano unaweza kuvunjika ndani ya serikali moja, mbili, tatu na hata tano"

Ujumbe wa UKAWA ni HIYARI. Ndiyo maana baadhi ya wajumbe kama ISACK CHEYO wali-walk out pamoja na UKAWA bungeni lakini keshoye walirejea na kuendelea na bunge.
Umoja huu unaheshimu haki wajibu na maamuzi ya kila mtu. Msimamo wa UKAWA ni kulinda na kutetea rasimu ya maoni iliyoletwa na tume ya mabadiliko ya katiba kwa msingi wa kulinda mamlaka na maoni ya wananchi.
Tutafanya kazi na mtu yeyote ambaye anaamini yale tunayoyasimamia. Hatutamuomba mtu yeyote asiyeona uzito wa hoja zetu atuunge mkono, badala yake tutaendelea kuwaheshimu wote wanaotofautiana nasi kwa hoja huku tukiendelea kupigania kile ambacho tunakiamini.
J. Mtatiro,
UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI(UKAWA),
Zanzibar.
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mutajiju; murudi bungeni musirudi sisi tunaendela

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duh we unaongeaje zaman wap?

      Delete
  2. Serikali 3 hamna katafuteni mapema nchi ya kuishi

    ReplyDelete
  3. Katiba ni ya wananchi walio wengi na wala sio ya viongoz ambao ni wachache na kwamsingi huo maoni ya wananchi ni LAZIMA ya sikilizwe.

    ReplyDelete
  4. akuna lolote nia yao ni kuvunja muungano kwan nchi wanachama watakuwa wakichangia asilimia ishirin kila mmoja hy aitosh wao nia ni kuvunja muungano kilicjo wapeleka zanzibar ni nin? kama sio uchochoze huo, mbn wao wameingia na kusgikilia hoja ya serikali tatu na wanaona wanashindwa wanasema wanarud kwa wananchi kuwaeleza nin wabunge walio weng ndio wanawsilisha wanancbi walio weng serilikal mbl ndio mpango wasilete sera za kihun hapa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wananchi na sio viongozi tunataka serikal 3 ndio kura ya maon inavyosema wewe mwenye jina lakike la kwanza!na nahis wewe sio mtanzania.

      Delete
  5. ukweli utabaki daima, ukawa wanatusaidia sana, nilichogundua watu weng wanataka serikali 3 lakin ni waoga hofu imewajaa tele

    ReplyDelete
  6. Wote mlio changia hapa niwasenge na mafala wakubwa.3lazma ipatikanike

    ReplyDelete
  7. Lazima tukubali kuwa kosa lilifanyika na baba wa taifa, kipindi wakati muungano unaasisiwa Mzee Karume alimtaka sana Mwl Nyerere kuwa muungano wetu uwe wa serikali moja lakini Nyerere alikataa, hakukataa kwa kukataa moja kwa moja ila hofu yake ilikuwa ni juu ya Wazanzibari kuja kusema kuwa Bara imewameza, hata hivyo licha tu ya kukataa Mwl Nyerere pia aliachia Zanzibar iendelee kutumia bendera yake, wimbo wake, na hata kuwa na rais wake, kitu ambacho kinaitambulisha kuwa ilibaki kuendelea kuwa ni nchi, kwani kinachoitambulisha nchi ni watu(Wazanzibari) bendera yake, raisi wake na mipaka. Watanzia sote ni wamoja kama ni makosa yalishafanyika, ila sio kigezo cha kulumbana sana, sisi wananchi tunachokitaka ni katiba mpya na sio mipasho bungeni, kama ni mipasho wangechukuliwa wabunge waimba taarabu!!!
    Tusitafutane jamani hii ni comment tu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad