UTAFITI:WANANCHI WANAUNGA MKONO RASIMU YA KATIBA YA WARIOBA

Utafiti uliofanywa hivi karibuni na Taasisi ya Twaweza umebainisha kuwa wananchi wanaunga mkono kwa kiwango kikubwa Rasimu ya Katiba iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa ikiongozwa na Jaji Joseph Warioba.

Ripoti ya utafiti huo uliofanyika Februari, mwaka huu kwa njia ya simu za mkononi na watu kuulizwa kuhusu mchakato wa Katiba, inaeleza kuwa kama wananchi wangeipigia kura rasimu hiyo mwezi huo, Katiba hiyo ingepitishwa kwa asilimia 65 Zanzibar na asilimia 62 Tanzania Bara.

Akiwasilisha ripoti hiyo jana, Mtafiti wa Twaweza, Elvis Mushi alisema kati ya watu waliohojiwa upande wa Tanzania Bara, asilimia 20 wangepiga kura ya hapana, kwa upande wa Zanzibar watu ambao wangesema hapana wangekuwa asilimia 19.

“Watu ambao walisema hawana uhakika na hawajui lolote kwa upande wa Zanzibar ni asilimia 19 na Tanzania Bara asilimia 15,” alisema.

“Zaidi ya asilimia 60 ya wapiga kura kutoka Tanzania Bara na Zanzibar walisema wana nia ya kupiga kura ya kuikubali Katiba (rasimu) kama ilivyo sasa.”

Muundo wa Serikali

Kuhusu muundo wa Serikali, Mushi alisema: “Asilimia 80 ya Wazanzibari wanaunga mkono muundo wa serikali tatu. Kwa Tanzania Bara wanaounga mkono serikali tatu ni asilimia 43.”

Alisema takwimu hizo ni tofauti na zilizotolewa miezi minane iliyopita ilipotolewa Rasimu ya Kwanza ya Katiba, ambayo asilimia 51 ya wananchi wa Tanzania Bara walipendekeza muundo wa serikali tatu.

Alisema baada ya kutolewa kwa Rasimu mbili za Katiba (ya kwanza na ya pili), Wazanzibari wanataka uhuru zaidi wa kujitawala au muungano wa serikali tatu, huku wananchi kutoka Tanzania Bara wakigawanyika nusu kwa nusu juu ya muundo wa serikali wanaoutaka.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Haya wale wa matusi wanaosubiria Udaku wapost udaku ili wapate nafasi ya kutukana.............vijana hoja za muhimu zinawapita na hamjui hata mfanye nn mnaangalia tu na kujadili umbea

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapo angeweka wema na daimond aah msg zingeshafika hata 30!vijana haya ndio mambo muhim y a ss kujadili hii katiba ni yetu wale ni wazee tu umri wao hauwezi hata ku last 15yrs from now!jaman tuijue na kuifaham kwa uhakika cos inatuhusu ss na vizazi vyetu vijavyo.

      Delete
  2. HAKUNA ANAEUNGA HOJA KW KUWA NI UONGO TAKWIMU HAZIJULIKANI

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad