ZAIDI ya vyama 10 vya siasa vya upinzani visivyo Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vyenye wajumbe katika Bunge Maalum la Katiba wamegoma kuunga mkono Ukawa baada ya kuamua kubaki ndani ya Bunge hilo kuendelea na mjadala wa Rasimu ya Katiba.
Ukawa wakiongozwa na mmoja wa viongozi wake, Profesa Ibrahimu Lipumba, juzi walitoka bungeni kwa madai kuwa, mjadala unaoendelea umekuwa wa matusi, ubaguzi na vitisho huku wajumbe wakilazimishwa kuridhia serikali mbili zisizo mapendekezo ya rasimu.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Samuel Sitta, leo alieleza kupata ujumbe wa uwepo wa wajumbe kutoka katika vyama hivyo na kuwatangazia wajumbe baada ya ombi kutolewa kwamba wajumbe walitaka kufahamu kama bungeni humo, wapo wanasiasa wa vyama vya upinzani.
Akithibitisha uwepo wa wajumbe wa vyama hivyo baada ya kukaribishwa kuthibitisha hilo na Sitta, Mwenyekiti wa Taifa wa chama cha APPT-Maendeleo, Peter Mziray alivitaja vyama hivyo kwa majina na wajumbe waliokuwemo bungeni walisimama.
“Mheshimiwa Mwenyekiti nashukuru kupata fursa hii kwamba mtambue tupo, kwanza niseme tu kwamba tutahakikisha Katiba inapatikana na nimepokea ujumbe wananchi wanawataka warudi, mambo yote yanamalizwa mezani,” alisema Mziray.
Miongoni mwa vyama vilivyotajwa kuwepo bungeni ni pamoja na Demokrasia Makini, ADC, Jahazi Asilia, Wakulima AFP, Tadea, UPDP, TLP, CCK, Chausta, Sauti ya Umma (SAU), UND na chama cha DP kinachoongozwa na Mchungaji Christopher Mtikila ambacho mjumbe mmoja alikuwepo.
Mziray alisema vyama vyao vina usajili wa kudumu na havitaondoka bungeni mpaka Katiba ipatikane kwa mujibu wa sheria.
Naye kiongozi wa UDP, Gidion Cheyo alisema wapo bungeni kujadili mustakabali wa nchi ndio maana pamoja na kwamba wengine wao ni Ukawa, hawakutoka bungeni.
hawana lolote hao posho tu
ReplyDeleteWanaendekeza siasa chafu na posho hawawezi kujitoa wananjaa sana wapumbavh hawatendi haki kwa wananchi na wako na ccm ndo maana hatujasikia wakisema sio wao nao ni ndio hata wakitiwa madole ndiooo
ReplyDeleteUKAWA WANATAKA SIFA 2
ReplyDeleteSifa wamtakie nan na ili wapate nin?hao wako kwa ajir ya kuwasaidia choka mbaya kama wew ambae hujui a wala be,upo upo we bora liende tu!kazi yao kubwa ni kuhakikisha Katiba iliyo bora na sio ya Kifisad inapatikana na bila wao wew leo sijui unge kuwa wap!ndio maana nasema huna unacho jua ungekuwa unajua ungetanguliza shukran!wale hawana shida majumban kwao walikuwa wanauwezo wa kukaa kimya bungen na posho ikaingia kama kawa!sasa eatake radhi usipo wataka ina maana wewe bado ni "mburula".
DeleteWanakusaidia nn, wanapiga kelele tu, hatuwezi pata chochote kwa kelele zao, tukiwapa nchi watatumaliza huku tunajiona
DeleteNa hawa ambao mmewapa nchi sasa ni miaka 52 na nchi bado iko vile vile na ufisadi ndio umejaa unasemaje?
Deletewe unaesema wananjaa kumamako
ReplyDeleteNJAA ZITAWAUA HAO
ReplyDeleteNingependa ipitishwe sheria ya kwamba chama chochote cha siasa kisipopata kiti cha ubunge au uwakilishi KIFUTWE.
ReplyDeletemaana kuna wengine hapo wanaishi kwa ruzuku tu.
hivyo cyo vyama vya upenzani, ni vyama vidogo dogo vya ccm, havina lolote njaa zao tu ndiyo zinawasulubu watanzania kuzidi kutawaliwa na mafisadi.
ReplyDeletekweli kaka ninjaa ndo ina sumbua afadhali ume ona kaka
Deletedah
Delete