WARIOBA ATOA YA MOYONI "MATUSI NA UONGO BUNGE LA KATIBA VINANIUMIZA"

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba amesema baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wametumia vibaya Bunge hilo kwa kumshambulia na kumsingizia mambo ya uongo kwa makusudi, akisema matusi yanayotolewa dhidi yake yanamuumiza.

Aidha, Warioba amesema ingawa haelewi kwa nini wanaomshambulia wameamua kutumia lugha za matusi dhidi yake binafsi, hatajutia kuchaguliwa kuiongoza tume hiyo kwa kuwa ilikusudia kuwaletea maendeleo wananchi wote kwa kuwapatia Katiba wanayoitaka.

Kauli hiyo ya Jaji Warioba imekuja wakati baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba na viongozi wa CCM wakiikosoa Rasimu ya Mabadiliko ya Katiba kwa maneno makali,huku wakimshutumu na kumkejeli yeye na baadhi ya wajumbe wa tume aliyoiongoza.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. umefanya ndivyo sivyo warioba shame on you why umelete takwimu za uongo kwa kuendelea kudhani watanzania bado ni wajinga hawana wanalolijua, kuendelea kudanganya kama mlivyozoea miaka yote mkajua ndo kila siku, watanzania wameamka na wanakili so umechemsha warioba, sana sana ni kula tu pesa kodi ya watanzania wenye hali ngumu, mana toka upewe mchakatowa tume mpaka leo ni muda gani umetumbua tu pesa, jamani watu wanauroho wa madaraka, kutudanganya serikali tatu zisizo na hoja wala ni vipi zinafanya kazi kisa uje uwe rais na mungano, jamani tufikie wakati wazee tuwachie vijana nao wawe viongozi, warioba wewe umekuwa kiongozi toka nyerere mpaka leo ni zaidi ya miaka 50 unatumbua tu pesa za watanzania walio wanyonge lkn hujatosheka mpaka leo bado unauroho wa madaraka wa kutaka kulitumbukiza taifa pabaya kisa upate serikali tatu uwe kiongozi wa mungano uendele kutumbua kodi za wananch, nasema hivi ifike wakati watu tuwe na hofu na mungu kwa kula pesa za walala hoi, muwe wazalendo kama nyerere na mandela kuamuakung'atuka na kuwanchia vijana washike uongozi.

    ReplyDelete
  2. Uliyekomment hapo wewe ndo mroho wa madaraka na hujui unachokiandika unajichanganya tu, mara uchu wa madaraka, mara serikali tatu, kwa nini wasingeiruhusu kama ilivyopendekezwa na wananchi irudi tena kwa wananchi waipigie kura wenyewe? Unabwabwaja tu hapo.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad