WATANZANIA WALIOLIPULIWA NA OSAMA KULIPWA Sh 672 BILION

Watanzania wanne waliojeruhiwa katika mlipuko wa bomu katika ubalozi wa Marekani mwaka 1998 na wengine watano waliofariki dunia katika mlipuko huo watalipwa fidia ya Sh672 bilioni, kiwango ambacho ni sawa na bajeti ya wizara nne za Tanzania.

Watanzania hao waliuawa na wengine kujeruhiwa katika moja ya mashambulizi pacha yaliyotokea kwa wakati mmoja jijini Dar es salaam na Nairobi, Kenya na ambayo yaliratibiwa na Osama Bin Laden akitumia mtandao wa kundi la Al Qaeda mwaka 1998 kwenye ofisi za balozi za Marekani.

Katika mashambulizi hayo yaliyotokea saa 4:00 asubuhi Agosti 7, 1998, Wakenya 200, Watanzania 10 na Wamarekani 12 walipoteza maisha na pia magaidi wawili nao walikufa.

Kati ya Watanzania 10, ni kesi za watu wanne tu waliouawa tu zilizofunguliwa kudai fidia ya watu hao kupoteza maisha.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Hata kama wangetoa mabilion zaidi ya hayo, bado thamani ya uhai wa binadamu huwez kufanisha na gharama ya chochote kile hapa duniani,

    ReplyDelete
    Replies
    1. toka 98 mpaka leo wengine waliokufa watalipwaje lol

      Delete
  2. Walikuwa wanaangalia mafanikio na muitikio baada ya hao kutolewa sadaka.
    wengi waliamini Osama ingawa ulinzi wa balozi hizi ulivyo juu.
    Akili kich..

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad