Ikiwa ni Siku ya pili tangu Wajumbe wa Bunge la Katiba Kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo,Cuf na NCCR Mageuzi wanaounda kitu kinachoitwa UKAWA wasusie Shughuli za Bunge la Katiba kwa Madai wamechoka Kutukana na Kuburuzwa kwenye Bunge hilo.
Hii leo Naibu waziri wa Fedha Mh:Mwigulu Nchemba ambaye kwa Sasa anakaimu Kuwa Waziri wa Fedha tangu Tarehe.10./04/2014 hadi 18/04/2014 kutokana na Waziri wa Fedha kusafiri Nchini Marekani Kikazi,amefuta Malipo ya wabunge waliosusia Mchakato wa Katiba.
Habari za Uhakika Kutoka Chanzo chetu ndani ya
hazina kinasema,Mwigulu Nchemba ameagiza Mabenki yote kurudisha Cheque za Malipo ya Posho na seating allowance zilizopelekwa na Bunge jana tar.16/04/2014 ili ziwekwe kwenye akaunti binafsi za Wabunge ikiwa ni Malipo ya Mpaka tar.30/04/2014.Pia ilikujiridhisha na taarifa hizo,Mwandishi wetu alizungumza na Wajumbe namna Mtiririko wa Malipo unavyofanyika ndani ya Bunge hilo,Mjumbe(Jina tunalihifadhi) alisema fedha zote zinapitia Benki na wakati wanajiandikisha siku za Kwanza walitakiwa Kuandika namba zao za Benki na Malipo yote hupitia huko,hivyo kama ni fedha zinazuiliwa Benki.
Baadhi ya wabunge wa CUF na Chadema wanaojiita UKAWA toka jana walijua wameshasaini fedha hizo hivyo zitaingia kwenye account zao Binafsi. Mambo yamekuwa tofauti baada ya Naibu Waziri wa Fedha(Sera) Mh:Mwigulu kuagiza leo form zisainiwe upya leo na zitasainiwa pia tar 22 mpaka 25,Kwa madai ya asiyefanya kazi na asile.
Mbali na hilo,Mh:Mwigulu amenukuliwa na clouds fm akisisitiza Rais kuwafuta wajumbe wakiojitoa na badala yake awateue watu waliotayari kutunga katiba hata bure kuliko hawa wanaokutana vikao lukuki kupanga njama za kususia mchakato. Aidha Mwigulu alisema fedha inayotumika ingeweza kulipwa Wazabuni wanaozidai halmshauri, wangeweza kulipa madeni ya walimu, au kuwapa mikopo watoto wa masikini waliofaulu ila hawajaenda vyuo kwa kukosa mikopo, au zingenunua madawa hosipitalini, au zingepeleka umeme, maji, vitabu au barabara lakini wamelipwa wajumbe badala ya kufanya kazi hiyo wanapanga njama ya kuhujumu mchakato usiendelee kwa kutafuta visingizio lukuki.
Bunge la Katiba linategemewa kuendelea Tar.22 Mwezi huu mara baada ya sikukuu za Pasaka Kupita na litaahirishwa tena Tar 25 mwezi huu kupisha Bunge la Bajeti la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Hivi wewe nchemba unadhani wenzio wanaishi kwa posho kama we we ulivyo mtumwa was posho? Mchumi mzima umeshindwa kujiajiri,.looh?
ReplyDeleteKwan nan kakwambia ye anaishi kwa posho...
DeleteHata kama ukizifungia hizo fedha zao haitakusaidia kitu wew mchumia tumbo!na wao sio kwamba wanashida na dhiki na hizo hela,wangekuwa na shida nazo basi wasingesusia kikao chenu mavi kilicho jaa ufisad na madudu ktk katiba yenu ya kichina hiyo,yaan nimesha sema na nitaendelea kusema mpaka UMA WA TANZANIA siku watanielewa ninacho maanisha,wew Mwigulu Mchemba wew sio kiongozi mzalendo kabisa wew ni mchumia tumbo ingawa unajifanya mwana harakat!wew ni mwana harakat wa mafisad lakin sio walala hoi,kama kweli una uchungu waambie hao Mafisad wenzio wazirudishe hela zetu zilizoko USWIS sio unakaa kujibaraguza unajifanya hela zingetengeneza shule hospital leo ndio unalijua hilo?wakati mikataba feki na hela za wana nchi zina tumika vibaya mbona husimam bungen ukasema hilo?wew utabak kuwa mchumia tumbo na mkosea heshima UMA WA TANZANIA....mtu kama wew ulitakiwa unyongwe hadhalan ni mtu mbaya sana wewe.
ReplyDeleteYani hakuna la nyongeza.umenena mdau.
DeleteHii haitaji kutoa kauli automatically kwahiyo walilipwa in advance huu ni upuuzi
ReplyDeleteBunge linaisha tar 25 april ila malipo mpaka tar 30 april
ReplyDeleteutakuwa ni ujinga na ndo maana wameondoka kwa kujigamba shwain kweli
DeleteHuyo waziri mtu wa ajabu sana,hao waliojitoa bungeni hawakwenda bungeni kwa ajili ya posho!Usifikiri kuwa watu wote wanaweza kununuliwa.Wasikilize hoja zao na wanataka nini,sio kufikiria ulaji,kama kuna mliowachagua kwa kuwanunua shauri yao wabaki na kuunga mkono.Swala la katiba ni gumu na linataka uwazi na kufikiri sio kama wewe ulivyochaguliwa na huyo waziri wako,kirahisi tu bila kuwa na sifa.
ReplyDeleteMbowe hana njaa,wala Maalim Seif wasikilize!
ReplyDeletewatakula
ReplyDeletejeuri yao
ccm juu
Mmmh amefanya cha maana kuzuia huo mkwaja coz inakuwa ni kama kuhujumu uchumi wa nchi.big up mwigulu
ReplyDeleteMwigulu hijifanya mzalendo sana kwa kuvaa scurf..........wizi mtupu
ReplyDeleteCCM sitakuja kuwapenda, mashetani ....
ReplyDeleteWe bwege nn kwao ccm inakupenda kwanza kujujua haikujui shobo tu
Deletewe acha mbwembwe safiiii sana mwigulu coz hawa wanaotoka bungeni ni wahuni tu.hawana jipya ccm hoyeeeeee,,,hapana chrzea ccm
ReplyDeleteMabadiliko na mwamko Tanzania,yameanza,serikali ya Tanzania inatawaliwa na CCM,na so utawala wa sheria,muda umefika ,taifa litambua,mambo ya miaka ya 1970,au miak ya 1980 hayata rudia katika historia ya Tanzania,muda si mrefu wako viongozi wataanza kushitakiwa katika historia ya nchi yetu,kwa kuwa wanasheria wa ndani ya nchi,na nje ya nchi Watanzania tumeona ,hilo ,nchi imekuwa kama shamba la babu,shwala la loliondo,mauaji ya wakulima na wafugaji,masoko ya tanzanite ,na mazao mengine,hayasimamiwi vizuri,kwa hiyo viongozi waliotumia muda wao vibaya wajiandae ,hata kama wako vyama vya upinzani ,sheria itawafuata,nchi yetu ,laini tunakuwa kama wakimbizi,hakuna ajira,polisi wanauwa wananchi,mikopo ya wanafunzi inapatikana kwa shida,wazee hawaheshimiwi,hkuna hata nyumba za kuhudumia wazee,walio simama kwa uaminifu kujenga hili taifa,vjana tumechoka kuona jinsi nchi inaliwa,bila huruma.
ReplyDeleteUhuru wa kuishi Tanzania ,sijui umekuwaje? polisi,wawe makini mkono wa sheria utawakuta ,kuwafukuza kazi ,kwetu haitoshi,mnapendelea wageni,badala ya wazawa,watu wa Serikali ya CCM,pia,muangalie hilo,masoko ya mazao yetu hayaeleweki,hospitali,mara mmenunua radar mbovu.masikitiko,Mungu atusaidie karne ya 21 bado ,hata viongozi wetu hamwaheshimu walio tukomboa kutoka kwa wakoloni,? hata siamini yanayotokea mbele ya macho yangu,mabomu ,viongozi wa dini,kuuawa, vijana amkeni kutetea nchi yetu na watu wake,kila mmoja asimame katika nafasi yake.