Afia Kaburini Baada ya Kunaswa na Kitu Akijaribu Kufukua ili Aibe Fuvu

Vyombo vya habari vya Nigeria vimeripoti habari ya mtu mmoja aliyekutwa amefia kaburini kwamba  alikubwa na umauti wakati akifanya jaribio la kufukua kaburi ili aibe fuvu la marehemu kwa ajili ya matumizi ya mambo ya kishirikina.

Kwa mujibu wa Saturday Tribune la Nigeria, tukio hilo limetokea katika mji wa Ilobu eneo oa Osun ambapo mtu huyo alikutwa akiwa amekufa huku nusu ya mwili wake ukiwa umeingia kaburini.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo ameeleza kuwa kijana huyo alikuwa na marafiki zake wengine waliokuwa wanafanya tukio hilo kwa lakini baada ya kuona mwenzao amenaswa ndani ya kaburi wakakimbia na kumuacha huku wao wakiwa salama.

“Mwili wake ulikutwa majira ya saa kumi na mbili na nusu asubuhi na kichwa chake kilikuwa kimefunikwa na tope. Wakazi wa eneo hili waliripoti polisi na walikuja baadae wakautoa mwili wake na kuuweka kwenye gari lao na kuondoka nae.” Alisema mkazi wa eneo hilo.

Saturday Tribune iliongea na kamishina wa Jeshi la Polisi wa eneo la Osun, Ibrahi Maishanu ambaye alieleza kuwa polisi watafanya uchunguzi wa kina kufuatia tukio hilo kufahamu nini hasa kilikuwa chanzo cha kifo chake. Na kwamba polisi hawajathibisha kuwa tukio hilo linatokana na masuala ya kishirikina

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wasitudanganye hapo kuna watu walienda kumfukia

    ReplyDelete
  2. Kweli bro wasitudanganye hao. Kitu gani hicho, kama kuna kitu kilichomkamata si wakitume kimkamate book haram.

    ReplyDelete
  3. waongo hapo inaonekana kenye karo na ciment inaonekana

    ReplyDelete
  4. Hiyo nayo kali

    ReplyDelete
  5. makaburini c mahali pa kuchezea, na cku zote uwez shindana na mungu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad