Ajabu:Mvua ya Samaki Yawapa Neema ya Kitoweo Raia

Afrika Mashariki na sehemu nyingine tumezoa kuwa kama mvua haitakuwa ya maji pekee basi itakuwa mvua ya mawe yanayotokana na barafu, lakini raia wa Sri Lanka wao wana uzoefu wa kukinga mvua ya samaki na kutumia kama kitoweo!
Wakaazi wa kijiji kimoja huko Magharibi mwa Sri Lanka wamekutwa na neema ya aina yake baada ya kunyeshewa mvua ya samaki wadogo wanaofaa kwa kitoweo.

Wakielezea tukio hilo, wanakijiji hao wamesema walisikia kitu kizito kikidondoka waligundua kuwa ni samaki, waliwakinga samaki hao na waliwapata wengi wenye uzani wa kilo hamsini ambao waliweza kuwatumia kama kitoweo.

Kwa mujibu wa BBC, Wanasayansi wameeleza kuwa mvua ya samaki hutokea wakati ambapo upepo mkali unakuwa juu ya maji ya kina kifupi na kusababisha mzunguko wa maji unaovuta karibu kila kitu kilicho ndani ya maji ikiwa ni pamoja na samaki na vyura.

Wameeleza kuwa viumbe hao wa majini wanaweza wakasafirishwa kwa masafa marefu na kushikiliwa na mawingu kwa muda hata baada ya ule mzunguko wa maji kuisha, na baadae wanashuka kama mvua.

Tukio la aina hii liliwahi kutokea Sri Lanka mwaka 2012 ambapo mvua ya samaki aina ya kamba wa baharini ilinyesha kwa mtindo huo.

Mvua hii ikinyesha vijijini huenda wanakijiji wakaomba iwe ya mafuriko ya samaki…anyways, ingekuwa vipi kama mvua inayonyesha sasa hivi Dar es Salaam ingekuwa mvua ya samaki wanaotumika kwa kitoweo?

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ivi mitandao yakijamii uongo mumezoeya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad