Amri Kiemba na Juma Kaseja ni Mungu Anajua

HALI ya mambo bado si nzuri kuhusiana na hatma ya wachezaji wawili mahiri ambao ni Amri Kiemba wa Simba na Juma Kaseja wa Yanga.

Yanga ilipanga kuachana na makipa wake wawili, Juma Kaseja na Ally Mustapha ‘Barthez’ na nafasi zao zizibwe na Aishi Manula wa Azam FC lakini dili hilo kwa sasa limeshindikana.

Barthez amemaliza mkataba wake na hataongezewa kwavile ameanza mazungumzo na Simba ambayo habari za ndani zinadai ameshapewa kopi ya mkataba wa miaka miwili lakini hajausaini, ila Kaseja bado ana mkataba Jangwani.

Habari za uhakika ambazo Mwanaspoti inazo ni kwamba Yanga imemshindwa Manula kwa vile bado ana mkataba wa miaka miwili na Azam, hivyo kumkosa kipa huyo imekuwa ni ahueni kwa Kaseja ambaye Yanga walikuwa wakifikiria kusitisha mkataba wake kutokana na mwenendo wake kutowaridhisha kwenye mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Habari za ndani zinasema kwamba Yanga kwa sasa watabaki na makipa wawili ambao ni Kaseja na Deo Munishi ‘Dida’ na ataongezwa kipa mwingine chipukizi.

Lakini huku Simba kama wakitii alichoagiza Kocha Mkuu Zdravko Logarusic huenda wakaachana na kiungo wao mahiri Amri Kiemba.

“Alitaka wachezaji 12 tu wabaki Msimbazi, kati ya hao jina la Kiemba halipo, ametupa kazi sisi kama kamati kuangalia kama aendelee au aachwe kulingana na jinsi tunavyomuona lakini kwake yeye kama atapatikana mtu mzuri zaidi, Kiemba atemwe,” chanzo cha uhakika kimeiambia Mwanaspoti.

Hata hivyo kigogo huyo wa kamati ya usajili aliongeza kuwa; “Tulilazimika kujadiliana lakini tumekubaliana Kiemba haendi kokote ni mzoefu sana na hatuwezi kupata mbadala wake haraka.”

Kiemba na Kaseja ni miongoni mwa wachezaji wazoefu na mahiri nchini ambao wameng’ara na timu za Taifa na wamezichezea Yanga na Simba kwa nyakati tofauti.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. bora kiemba, kaseja atumtaki live bila chenga

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad