Arsene Wenger Asingedumu Hispania Kama Angekuwa Kocha kwenye Ligi Hiyo

KOCHA Mkuu wa West Brom, Pepe Mel amesema kocha Arsene Wenger kushindwa kutwaa mataji kwa muda mrefu huku akiwa na kikosi imara kama cha Arsenal ana bahati sana kwa sababu kazi yake anafanya England na kama angekuwa Hispania angefukuzwa kazi siku nyingi.

Arsenal haijatwaa taji lolote la maana tangu mwaka 2005 ilipotwaa Kombe la FA na msimu huu wanaweza kumaliza ukame huo kama wataifunga Hull City kwenye fainali ya Kombe la FA itakayofanyika Mei 17 uwanjani Wembley, London.

Mel anasapoti falsafa za kocha huyo Mfaransa, lakini anashangaa ni vipi anakinoa  kikosi chenye wachezaji makini kama cha Arsenal na kushindwa kunyakua mataji.

Wakati Gerardo Martino akijiandaa kuondoka Barcelona mwisho wa msimu, Wenger anapewa nafasi ya kurithi mikoba, lakini Mel anamtaka aendelee tu kubaki England kwa sababu kama atakwenda Hispania hatadumu kwa muda mrefu kwa kuwa na timu isiyotwaa mataji.

“Sidhani kama Arsene angeweza kudumu na kibarua chake nchini Hispania,” alisema Mel, 51.

“Carlo Ancelotti ni mfano mzuri pale Real Madrid. Miezi mitatu iliyopita alikuwa kwenye presha kubwa sana kabla ya sasa kupoa kwa sababu ameifikisha timu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Hispania kocha anaishi kutokana na matokeo.”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad