Baada ya Kikombe cha Babu, dhahabu yaibuka Samunge

Maelfu ya watu wamemiminika tena katika eneo la Samunge, Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha, safari hii siyo kunywa Kikombe cha Babu Mchungaji Ambilikile Mwasapile, bali kupata dhahabu inayodaiwa kugundulika  katika eneo hilo.

Habari kutoka katika eneo hilo zinasema kuwa watu wanazidi kumiminika katika kujipatia madini hayo yaliyobainika katika mashamba ya watu na maeneo ya kingo za Mto katika Kijiji cha Mgongo kilichopo jirani na Kwa Babu.

Diwani wa Samunge, Jackson Sandea alisema maelfu ya watu kutoka maeneo mbalimbali nchini wamefurika katika kijiji ambacho kuna mto na madini ya dhahabu yanapatikana hapo.

“Hadi sasa kuna watu zaidi ya 4,000 na bado wanaongezeka, hii inaweza kuwa ni zaidi ya kipindi kile cha Babu wa Kikombe. Dhahabu hii inapatikana mtoni tu, watu wanakusanya michanga na kupata dhahabu, hakuna mtu ambaye anachimba,” alisema Sandea.

Alisema tofauti na maeneo mengine, dhahabu ya Samunge inaonekana ni ya Watanzania wote kwani ipo eneo la mto ambao unamilikiwa na Serikali na ndiyo sababu watu wanaingia kwa wingi.

“Kuna wengine wanapata hata mashambani lakini mtoni ndipo inapatikana kwa wingi zaidi,” alisema.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. uyu babu wa samunge nna mashaka nae... Lucifer

    ReplyDelete
    Replies
    1. Daaaaaah kweli kabisaaaa haiwezekani dhahabu zimiminike kwenye mto! au wanataka mto utanuke.

      Delete
  2. Ni nyakati za mwisho,anyone who has studies the bible will recognize this.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahah "has studies" imekuchefua bwana negro peligro.

      Delete
  3. Tatizo wameshapiga kelele, kesho tu Prof Muhongo atawauzia wazungu halafu hao wanaoshangilia wataambiwa hawana uwezo wa kuchimba, na pili kiukweli wanaharibu mazingira maana wanachimba hovyo hovyo...

    ReplyDelete
  4. babu huyu si wakawaida namchukia toka adanganye umma wa watu kwamba anatibu ukimwi na maelfu kwa malaki ya watu wakateketea, isije watakaoenda kuchimba hizo dhahabu wakapoteza maisha yao, babu mwanga na nguvu za giza, kanisa lake wanaswali milimani uchi, unategemea nini pigine kafara la kikombe limeisha sasa dhahabu watakao chimba sasa watakufaje namchukia kwa kuwa muongo anamsingizia mungu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad