Bibi anaswa amebeba ‘unga’ Uwanja wa Ndege Dar

Dar es Salaam. Bibi mmoja raia wa Nigeria, Olabisi Ibidun Cole (65) amevunja rekodi ya umri wa watu wanaokamatwa wakiwa na dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Cole alikamatwa Jumatatu akiwa amemeza kete 82 aina ya heroini zilizokuwa zimefungwa kwenye karatasi zinazofanana na ganda la sigara, ambazo si rahisi kuonekana katika mitambo.

Habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya, Alfred Nzowa zimesema pamoja na mbinu zake na kujiamini, mwanamke huyo alikamatwa kutokana na ushirikiano wa vitengo mbalimbali vya uwanja wa ndege.

Kamanda wa Polisi wa Uwanja wa Ndege, Hamisi Selemani alisema mwanamke huyo alikamatwa Mei 19, mwaka huu saa tisa alasiri akijiandaa kwenda Paris, Ufaransa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia.

Selemani alisema raia huyo aliwasili nchini Mei 15, mwaka huu na alikaa muda wote bila ya kuwa na shughuli yoyote, jambo ambalo lilitiliwa shaka na kumkamata.

“Huyu mwanamke achana naye, akisimama mbele yako huwezi ukaamini kwa jinsi anavyojiamini. Alikuwa na mbinu mpya ya kufunga hizo kete. Kila moja ilifungwa kwa karatasi inayofanana na ganda la sigara,” alisema Selemani.

Alisema mwanamke huyo alitumia mbinu hiyo ili asigundulike wakati akikaguliwa kwa mitambo maalumu inayogundua dawa za kulevya.

Taarifa zaidi zinasema kuwa kutokana na mbinu yake ya ufungaji wa kete, mwanamke huyo alikuwa tayari amevuka hatua ya kwanza ya ukaguzi.

Nzowa alisema baada ya kumhoji, mtuhumiwa huyo alidai kuwa aliingia nchini kwa ajili ya kutafuta soko la kuuza vipodozi na nguo.

“Wakati tukiendelea kumhoji, Kikosi Kazi cha Kuthibiti Dawa za Kulevya kilibaini na kugundua kuwa alikuwa amemeza dawa za kulevya.

“Huyu ni mzee, lakini tumeshangaa kuona bado ana nguvu za kutosha na tulishangaa baada ya kutoa kete 20 kwa mara moja katika awamu ya kwanza, jambo hili si rahisi kutokana na umri wake,” alisema Nzowa.

Mtuhumiwa huyo aliyekuwa na hati ya kusafiria ya Nigeria, anaendelea kuhojiwa na upelelezi ukikamilika atafikishwa mahakamani.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bongo supu. Wacha ss akafie jela

    ReplyDelete
  2. Baada yakulea wajukuu angalia sasa kilichomkuta,majuto ni mjukuu.

    ReplyDelete
  3. Baada yakulea wajukuu zake,angalia ss yaliomkuta,kabaki na majuto ni mjukuu.

    ReplyDelete
  4. hahahaaa.... Mdau ati majuto c mjukuu.... Acha akome maana ndugu zake wanabaka wabongo china na kuwaua au kuwaua nakisha kuwatoa kiungo cha mwili

    ReplyDelete
  5. wanawala sangi wabongo

    ReplyDelete
  6. Polisi wa bongo bwana eti upepelezi ukikamlika atafikishwa mahakamani..sasa hapo kuna upelelezi gani?..acheni mbereko nyie mpelekeni akapigwe nyudo zake

    ReplyDelete
  7. hao polisi njaa,,, na hayo madawa baada ya kumkamata wanayapeleka wapi?,

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad