Bolti Aomba Msaada wa Kupatikana Viatu vyake Vilivyoibwa Uingereza

Bingwa wa Olympic wa mbio fupi Usain Bolti, ametoa taarifa za kupotelewa na viatu vyake vyenye thamani ya paund za kiingereza elfu ishirini.
Usain Bolti, ametoa taarifa hizo kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa twitter yenye watu million 3 kwa kumtaka yoyote alieviona viatu hivyo amrejeshee.

Bolti amelazimika kutangaza hadharani taarifa hizo, baada ya kuona hakuna muelekeo wowote wa kupatikana kwa viatu hivyo vyenye rangi ya machungwa sambamba na chapa ya kampuni ya Puma.

Tayari wapelelezi wa Scotland Yard wamethibitisha kwamba viatu hivyo viliibwa juma lililopita katika, mtaa wa Craydon mjini London maeneo ya viwandani ambapo viliwekwa kama maonyesho.

Hata hivyo licha ya viatu hivyo kuchukulia Usain Bolti, ameweka saini katika viatu vingine vitakavyopelekwa katika maonyesho hayo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad