Bunge la Bajeti Laanza Leo kwa Posho Mpya

Dodoma. Bunge la Bajeti linaanza leo mjini Dodoma huku wabunge wakitarajiwa kuanza kulipwa viwango vipya vya posho, ambazo ni Sh300,000 kwa siku sawa na kiwango wanacholipwa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba.

Kabla ya kufikia uamuzi wa kupandisha viwango hivyo kwa Sh100,000 zaidi, wabunge walikuwa wakilipwa Sh200,000 kwa siku (yaani Sh70,000 kama posho ya kikao (sitting allowance), Sh80,000 posho ya kujikimu (perdiem) na Sh50,000 ya gharama za usafiri).

Nyongeza hiyo kwa kila mbunge kwa siku, sawa na asilimia 50, italigharimu Bunge la Jamhuri ya Muungano kiasi cha Sh18.5 bilioni kwa siku 52 zilizotengwa kwa ajili ya Bunge la bajeti linalotarajiwa kuhitimishwa Juni 27.

Januari mwaka 2012, Rais Jakaya Kikwete alikataa maombi ya Bunge ya kutaka nyongeza ya posho ipande hadi Sh330,000 na badala yake wabunge hao wakapata nyongeza ya Sh50,000 tu kwa ajili ya usafiri.

Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililla alipoulizwa kuhusu nyongeza hiyo, hakuthibitisha wala kukanusha, lakini akafafanua kwamba hilo ni suala la uongozi wa Bunge na si la kiutendaji.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. yani wanazidi kujiongezea posho tu, lkn tukisema kiwango cha chini cha mshahara kiwe laki tatu mnaona mamilioni, kodi yenyewe hamkatwi, hivi hi ni halali jamani

    ReplyDelete
  2. Mmmh dunia ngumu

    ReplyDelete
  3. Ama kwel 2po kwenye dunia ya wenye nacho wataongezewa na wenye vichache watanyang'anywa hata hvyo vichache walivyonavyo.Tuombe tu neema ya Mungu

    ReplyDelete
  4. bunge la tz mbona kama magumashi posho zenu mnaziona bungeni mnaenda kuzinguana nishidaaaaah ila hatutaki wabunge vilaza mnalala 2!!!

    ReplyDelete
  5. Itabidi 2piganie ubunge una raha..

    ReplyDelete
  6. Serikal nzuri hii inajali viongozi wake!wananchi aaah kivyenu nyinyi subirini kupanga folen kwenye jua kali na kuwapa kura ili wakale!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad