CCM ‘kuishambulia’ Ukawa Kwa Siku 26

Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wanaanza ziara ya siku 26 katika Mikoa mitatu ya Tabora, Singida na Manyara kukagua uhai wa chama na maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa baadaye mwaka huu.
Hata hivyo, duru za kisiasa zinaonyesha kuwa ziara hiyo ni sehemu ya kuushambulia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), ambao walitoka bungeni wakati wakijadili mchakato wa Katiba Mpya wakidai kutoridhishwa na mwenendo wa Bunge hilo. Ukawa pamoja na CCM walikwishafanya hivyo Zanzibar.

Wakati Kinana akifanya ziara katika mikoa hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Wazazi wa CCM, Abdallah Bulembo amekwishaanza kushambulia Mikoa ya Kusini, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Njombe na Iringa.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nauye alisema Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana ataanza ziara yake Mkoa wa Tabora, ambako atatembelea wilaya zote kuanzia Mei 8 hadi 18. Mkutano wa kwanza utaanza leo katika Wilaya ya Igunga.

Baadaye ataendelea Mkoa wa Singida kuanzia Mei 19 hadi 26 na kumalizia Mkoa wa Manyara, ambako ataanza Mei 26 hadi Juni 3 mwaka huu.

Nape alisema pia kuwa wamemkabidhi Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ripoti ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika Mikoa ya Kigoma, Rukwa na Katavi ili afahamu changamoto za mikoa hiyo.

Nape alisema kuwa ripoti hiyo inahusu changamoto na mafanikio ambayo yamebainika katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Kinana aliyoifanya hivi karibuni katika mikoa hiyo.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. upuuzi mtupu

    ReplyDelete
  2. There are so many problems the people are facing in there daily life,they have become permanet which means the present system of governance,leadership or goverment is not capable of solving them.Instead of talking about these problems we are so much engaged in talking about madaraka so they can continue to expolit and leave people with povrety and kunyanyaswa.We Tanzanianians we want to be given equal opportunities and social mobility.We have been waiting for so long tukadhani katiba mpya labda itafanya hivyo instead people are using it as a means of earning allowances draining the pockets of poor workers.Infact we need a social revolution which the present system is note capable.

    ReplyDelete
  3. mNATUZINGUA,HATUTAI SIASA TUNATAKA KUONA MAENDELEO WA VITENDO....SFOR SO LONG HAMJATUSAIDIA KITU KAZI KUPIGA DOMO TUU....

    ReplyDelete
  4. Atuna iman na serikal yetu kiufupi tumeichokaaa.....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad